JINSI MGOMO WA MADEREVA ULIVYOMALIZIKA TANZANIA

Hatimaye mgomo wa madereva umemalizika baada ya kufikia makubaliano kati yao na serikali juu ya namna ambavyo madai yao yatakavyoshughulikiwa na serikali.



Awali kabla ya kufikia makubaliano hayo askari walianza kutoa baadhi ya mabasi chini ya ulinzi mkali wa polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia FFU pamoja na askari wa usalama barabarani zoezi ambalo baada ya muda lilionekana kukwama kwa kile baadhi ya madereva waliokuwa kituoni hapo kudai kuwa mgogoro huo hauwezi kumalizika kwa kutumia nguvu.
 
 
 
Harakati za kumaliza mgomo huo zilianza mapema alfajiri kwa vikao vilivyofanyika kituoni hapo kati ya madereva na wamiliki wa mabasi na baadae mchana alifika mkuu wa wilaya ya kinondoni ambaye kabla ya kufikia muafaka huo wakiwa katika mazungumzo vurugu zilizuka gafla ambapo baadhi ya vijana walianza kurusha mawe kuelekeza kwa viongozi hao wakiwemo wakuu wa polisi na waandishi wa habari na baadhi ya watu kujeruhiwa hali iliyowalazimu polisi kutumia mabomu ya machozi.
 
 
 
Mara baada ya kufikia makubaliano hayo katibu wa chama cha madereva akazungumza na umati wa madereva na abiria waliokuwa kituoni hapo na kutaja madai waliotiliana saini na serikali huku mkuu wa wilaya ya kinondoni akielezea namna serikali itakavyoshughulikia suala hilo na yeye atafanya nini endapo halitafanikiwa.
 
 
 
Hata hivyo baada ya mabasi hayo kuanza kutoka ndani ya kituo hicho baadhi yake yalionekana kutokuwa na abiria ndani halikadhalika idadi kubwa ya mabasi yakibakia ndani ya kituo hicho.
 
 
 
Kufuatia mgomo huo uliotikisa nchi kutokana na mamia ya wasafiri kukwama maeneo mbalimbali ya nchi huku abiria wanaotumia usafiri wa daladala wakilazimika kutembea kwa miguu baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wamefika kituo kikuu cha mabasi ubungo na kuzungumza na abiria pamoja na madereva hao akiwemo Mwenyekiti chadema Freeman Mbowe na Prof Ibrahim Lipumba Mwenyekiti CUF nahivyo shughuli kuanza na dala dala kufanya safari zao kama kawaida.
Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post