ANGALIA PICHA- ASILIMIA 50 YA BARABARA ZA MANISPAA YA SHINYANGA ZIMEOZA!!

Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akishangaa shimo kubwa katika moja ya barabara ya kata ya Kitangiri(Sokoine Road)
Leo na meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam (kushoto)ameanza ziara ya  kutembelea barabara za kata za manispaa hiyo kujionea hali halisi ya miundombinu ya barabara  katika manispaa hiyo ambapo ametembelea kata 8 kati ya 17 ambazo ni Kolandoto,Ibadakuli Kitangiri,Ndala,Kambarage,Mwawaza,Masekelo,Ngokolo na


Mhandisi wa barabara katika halmashauri ya manispaa ya Shinyanga George Medard aliyekuwa ameambatana na meya wa manispaa ya Shinyanga Gukam Hafeez Mukadam akiwa katika barabara ya  Kolandoto -Galamba katika kata ya Kolandoto wakati wa ziara ya  kutembelea barabara za kata za manispaa hiyo kujionea hali halisi ya miundombinu ya barabara  katika manispaa hiyo ikiwa ni maazimio ya kikao kilichopita cha baraza la madiwani wa manispaa hiyo.Medard alisema changamoto inayowakabili ni ufinyu wa bajeti
Hapa ni Katika kata ya Ibadakuli-Katikati ni diwani wa kata hiyo Leonard Mayunga akimwonesha meya huyo jinsi barabara ya  Ugweto-Ipeja ilivyo korofi hivyo kuhitaji msaada wa haraka ili barabara hiyo pamoja na ile ya Ibadakuli-Uzogore zitengenezwe ili kuwaondolea kero wananchi


Hii ni barabara ya  Ugweto-Ipeja miongoni mwa barabara mbovu katika manispaa ya Shinyanga ambapo meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam anasema asilimia 50 ya barabara zote za halmashauri ya manispaa ya Shinyanga zimeharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hali inayosababisha usumbufu kwa watumiaji wa barabara hizo.


Diwani wa kata ya Ibadakuli Leonard Mayunga akimsisitiza meya juu ya umuhimu wa kutengeneza barabara akiomba zitengwe fedha za dharura kunusuru barabara za manispaa hiyo 


Hapa ni katika kata ya Kitangiri-Katikati ni diwani wa kata hiyo George Kitalama akionesha moja ya barabara katika kata hiyo inayoendelea kujengwa ingawa barabara nyingi katika kata hiyo kubwa ni mbovu na nyingi hazipitiki kutokana na mashimo na zingine kukatwa na maji ya mvua


Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akishangaa shimo kubwa katika moja ya barabara ya kata ya Kitangiri(Sokoine Road)


Diwani wa kata ya  Kitangiri George Kitalama akionesha barabara zake mbovu


Hapa ni katika barabara inayotenganisha kata ya Ndala na Masekelo lakini pia inakwenda hadi kata ya Masekelo,barabara ambayo ni korofi pia,imebomolewa na maji ya mvua huku mashimo ya kila aina yakitawala


Meya wa manispaa hiyo amesema  kutokana na bajeti kuisha hivi sasa wanajipanga namna ya kusaidia miundombinu hiyo irudi katika hali ya kawaida ingawa hali katika baadhi ya barabara inaridhisha.


Barabara hiyo ikiwa imemomonyoka


Meya akijadili jambo na mhandisi wake


Barabara kuelekea kata ya Mwawaza karibu na panapojengwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga


Hapa ni katika daraja la Mto Ndama-daraja ambalo limejengwa na mkandarasi Mega Teck wa Tanga,hii sehemu inaelezwa kuwa ilikuwa korofi hivyo manispaa ya Shinyanga imeondoa changamoto hiyo sasa wananchi wanapita kwa raha kama unavyoona pichani


Muonekano wa daraja hilo


Mhandisi wa barabara katika halmashauri ya manispaa ya Shinyanga George Medard  akiangalia daraja la mto Ndama


Hapa ni katika kata ya Kambarage- Katika barabara ya Kambarage-Ndala,barabara ikiwa imeharibika vibaya


Hapa ni katika kata ya Ngokolo-Meya akiwa katika shimo kubwa karibu na Hotel nyingi za eneo hilo karibu na ofisi ya afisa mtendaji wa kata hiyo


Ndiyo muonekano wa barabara za manispaa ya Shinyanga


Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akizungumza katika kata ya Ngokolo ambapo amesema kabla ya mvua barabara nyingi zilikuwa nzuri na zenye kiwango na baada kuanza sura nzima ya manispaa ikabadilika kutokana na barabara kukatika na kuwepo kwa mashimo mengi barabarani.


Aliongeza kuwa  kutokana na bajeti kuisha hivi sasa wanajipanga namna ya kusaidia miundombinu hiyo irudi katika hali ya kawaida ingawa hali katika baadhi ya barabara inaridhisha.

Gulam alisema tayari ameshazungumza na injinia wa manispaa ya Shinyanga na sasa wanatafuta mafuta kwa ajili ya kutumia greda la manispaa hiyo na kwamba wanafanya jitihada za kuomba pesa za dharura kutoka bodi ya barabara ili ziwasaidie kujenga barabara hizo.Alisema barabara zingine zitajengwa kwa mradi wa benki ya dunia.

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post