MTOTO AUAWA KWA KUPIGWA MATEKE BAADA YA KUINGIZA MIFUGO KWENYE SHAMBA LA MTU HUKO KISHAPU


Mtoto mmoja aliyejulikana kwa jina la Masele Nyorobi(14) mkazi wa  kijiji cha Mwigumbi kata ya Mondo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga ameuawa kwa kupigwa mateke baada ya kuingiza mifugo katika shamba la mahindi na choroko la mkazi wa kijiji hicho.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha amesema tukio hilo limetokea Mei,01 mwaka huu saa sita mchana katika kitongoji cha Bulahu,kijiji cha Mwigumbi wilayani Kishapu ambapo Masele Nyorobi aliuawa kwa kupigwa mateke sehemu mbalimbali za mwili wake na Mwandu Masanja.

Kamanda Kamugisha amesema chanzo cha tukio hilo ni marehemu kuingiza mifugo katika shamba la Mwandu Masanja mabapo mifugo hiyo ilishambulia mahindi na choroko shambani humo.

Ameongoza kuwa mwili wa marehemu uligunduliwa na Nyorobi Njiku(53) mkazi wa Mwigumbi baada ya mtuhumiwa kufanya mauaji na kutokomea kusikojulikana.


Amesema jeshi la polisi linaendeleana juhudi za kumtafuta na kumkamata mtuhumiwa huyo huku akitoa wito kwa wananchi kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo.
Na Kadama Malunde-Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post