BOTI YAUA MMOJA ,WAWILI HAWAJULIKANI WALIPO HUKO PEMBA


Mtu moja amepatikana akiwa amefariki dunia kati ya watu watatu walio zama baharini baada ya kupinduka na FAIBA BOT huko Wesha katika wilaya Chake Chake huku ikiwa watu wawili bado kupatikana hadi zoezi la uokozi lilipo fungwa rasmi hivi leo.


Wakitangaza kufunga kwa zoezi hilo uongozi wa Mkoa Kusini Pemba kamanda wa polisi mkoa Kusini Pemba Juma Yusufu Ali na mkuu wa mkoa huo Bimwana Juma Majid Abdalla walio kuwepo eneo la tukio wamesema kazi ya uokozi ilikwenda kwa kasi na kufanikiwa kupata mtu moja akiwa amekwisha fariki huko bandarini Mkumbuu .

Wamemtaja aliyepatikana kuwa ni Ali Mbarouk Salehe (55) mkazi wa Mitamani Chake Chake na wale ambao bado hawaja onekana kuwa ni Rashid Zahor na Omar Najimu Kibete wote wakaazi wa Mkoroshoni.

Akizungungumzia tukio hilo mmoja wa manusura wa ajali  hiyo aliye kuwemo ndani ya boti hiyo Ahmed Nasor 5(2) amesema jitihada za kutaka kuwaokoa wenzao hao ilifanyika ila kwa vile hakukuwa na chombo karibu  ndiyo ilipelekea wenzao hao kupotea.

 Naye moja wa waokozi  amesema wamefanikiwa kupata vifaa walivyokuwa navyo watu hao baada ya kuzamia katika boti yao ambayo ipo chini ya bahari na walipoikagua hakuna mtu hata moja.

Jitihada kubwa za kuwatafuta ilifanyika katika mwambao wa bahari ya eneo la Pemba Chanal walipozama watu hao kwa kutumia boti ngalawa watembea kwa miguu kwenye mikoko na ndenge aina ya chata ambayo imezunguka hadi mwambao wa Tanga.
Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post