KAMPUNI YA ACACIA YAONESHA BIDHAA ZAKE MAONESHO YA VIWANDA VIDOGO VIWANJA VYA SHYCOM SHINYANGA


Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Dhahabu ya ACACIA inayomiliki migodi ya Bulyankulu na Buzwagi mkoani Shinyanga leo imeonesha bidhaa na shughuli mbalimbali wanazozifanya katika migodi yao katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga ambako maonesho ya Viwanda Vidogo kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa yanafanyika na kilele chake kitakuwa Juni 2,2015.

Pichani kulia ni afisa Uhusiano mgodi wa Buzwagi Yunia Wangoya akimkaribisha mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga alipotembelea Banda lao namba 31 ,kwa niaba ya waziri wa Viwanda na Biashara nchini.

Afisa Uhusiano mgodi wa Buzwagi Yunia Wangoya akizngumza,ambapo alisema mbali na kujihusisha na shughuli za uchimbaji madini kampuni ya ACACIA pia inajihusisha na shughuli za utunzaji mazingira na shughuli mbali za kijamii.Aliyesimama mwenye tisheti nyeupe ni katikati ni mkurugenzi wa SIDO nchini Injinia Omary Bakari

Afisa Uhusiano mgodi wa Buzwagi Yunia Wangoya akimuonesha mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga miche ya miti inayooteshwa na kikundi cha Twikondele katika mgodi wa Bulyankulu
Kikundi cha upandaji miche ya miti ya mbao na matunda cha Twikondele wakiwa kwenye banda la ACACIA


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akiwa katika banda la ACACIA
Vijana wa kikundi cha Ufyatuaji matofali ya kufungamana cha Buzwagi wakionesha jinsi wanavyofatua matofali.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akiangalia jinsi vijana wa kikundi cha Ufyatuaji matofali ya kufungamana cha Buzwagi wanavyofatua matofali.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akiangalia kilichokuwa kinajiri katika banda la ACACIA

Maonesho yanaendelea
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akisisitiza jambo

Banda la ACACIA-Kikundi cha Asali cha Mwendakulima katika mgodi wa dhahabu wa Buzwagi wakiwa na asali yao
Asali kutoka mgodi wa Buzwagi

Bidhaa mafuta yanayotokana na asali

Kikundi cha Tupendane cha mgodi wa  Bulyankulu wakionesha sabuni za miche na maji katika banda la ACACIA

Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post