Maskini!! BIBI AMCHOMA VISU VYA MOTO MJUKUU WAKE KISA KAPOTEZA PENI (Kalamu) YA SHILINGI 200.


Jeshi  la  Polisi  Mkoani  Mwanza  linamshikilia  bibi  mmoja  aitwaye Laurencia  Athanas  mkazi  wa  Kiseke, Ilemela  jijini  Mwanza kwa  tuhuma  za  kumchoma  visu  vya  moto mjukuu  wake  na  kumsababishia  majereha  mbalimbali  mwilini  akimtuhumu  kupoteza  peni (kalamu) ya  shilingi 200.

Mtoto  huyo  aitwaye  Jackson  Hosea ( 10 )  ambaye  ni  mwanafunzi  wa  darasa  la  tatu  katika  shule  ya  msingi  Kiseke iliyoko  Ilemela  Jijini  Mwanza alifanyiwa  unyama  huo  nyumbani  kwa  bibi  huyo  ambaye  ni  mzazi  wa  mama  yake  aishiye  Nzega  siku  ya  Ijumaa  jioni   tarehe  23 Mei  2015.

Afisa  Mtendaji  wa eneo  hilo, Bi  Hellen  Mcharo  ameithibitisha kutokea  kwa  tukio  hilo  na  kudai  kwamba  liliibuliwa  kwa  mara  ya  kwanza siku  ya  Jumatatu  ya  Mei 25, 2015   na  mwalimu  wa  mtoto  huyo  aliyemtaja  kwa  jina  moja  la  Mwl. MidaliVia>>Mpekuzi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post