Hatari Sana!! BASI LA DAR EXPRESS LATEKETEA KWA MOTO HUKO PWANI!!,ANGALIA PICHA NA VIDEO LIKIUNGUA MOTO


Muonekano wa basi la Dar Express likiteketea kwa moto leo mchana eneo la Kwamakocho, Kijiji cha Kimange, wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.

Linahesabika kama tukio jingine la Basi kuwaka moto katika rekodi za mabasi yaliyowaka moto yakiwa safarini nchini Tanzania wakati yakiwa na abiria.

Taarifa zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Pwani SACP Jafari Ibrahimu ni kwamba basi hilo la kampuni ya Dar Express liliwaka moto likiwa safarini kutokea Dar es salaam kuelekea Arusha likiwa limejaa abiria.


DX 4Amesema >>> ‘Ni kweli basi la Dar Express saa saba mchana kwenye kijiji cha Kimange ndani ya Wilaya ya Bagamoyo Pwani lilipata hitilafu likaanza kuungua lenyewe, bahati nzuri abiria wote wamewahi kushuka salama ila basi limeteketea lote, hawakuwahi kulizima, hakuna yeyote aliejeruhiwa‘


Kamanda Ibrahimu amesema kuwa abiria wote waliokuwemo ndani ya basi hilo wako salama.

Eneo la Kwamakocho lipo katikati ya eneo la Mandela na Mbwewe mkoani Tanga.

RPC Jafari Ibrahimu amesema chanzo cha moto huo bado hakijajulikana na akasema uchunguzi unaendelea.

TAZAMA VIDEO HAPA UONE JINSI BASI LILIVYOKUWA LINATEKETEA KWA MOTO

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post