Picha na Video!! KUTANA NA GARI HII YA AJABU,UNAWEZA KUIKUNJA KAMA MWAMVULI!!,FOLENI HAZIKUPI SHIDA KABISAA!!

KAGARI
Kuna malalamiko ya foleni kwenye miji mikubwa Duniani, hii ishu hata Dar ipo pia.. ukiacha hilo kuna ishu ya parking.. inawezekana umejenga au unaishi kwenye nyumba yako ya kawaida kabisa lakini una changamoto wa wapi pa kupaki gari yako !!
KAGARI GERMANY

Timu ya wataalamu wakiwa kwenye gari ambalo wamebuni.. kwao itakuwa ni BIG DEAL kama dunia itaikubali hii teknolojia mpya.

Teknolojia haiko mbali na sisi kila siku, ubunifu unaofanywa hautaacha wakati mwingine kutushangaza pia.. timu ya Engineers Ujerumani wamefanya ufundi wao, wamekuja na hii gari ndogo ndogo yani.. na bado ina uwezo wa kubonyea ikawa ndogo zaidi.

Hii gari ni ya umeme, ina uwezo wa kusafiri mpaka kilometer 70 kwa battery yake ikiwa full charge kabisa !! Kingine ni kwamba ina uwezo na kupungua upana wake kwa kama centimeter 80 hivi, tyre zake pia zinageuka upande wowote unaotaka sio kama gari nyingine.. kama sehemu ya parking ni ndogo haitoshi basi hii inajipenyeza na inatosha kabisa.

Wapo waliovutiwa na ubunifu huu, Kampuni ya Mercedes Benz wao wamethibitisha kuipenda hii, ndani ya miaka 4 ijayo watakuwa na gari ambalo litakuwa na muundo kama huu.. General Motors pia wamesema mpaka 2020.


Video yake unaweza kuiona hapa..

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post