MSIMAMO HUU WA LIGI KUU SOKA TANZANIA BARA,UMEAMUA TIMU HIZI 2 KUSHUKA DARAJA,MATOKEO YA MECHI 7 ZA LEO YAKO HAPA PIA




 Leo Ligi Kuu Tanzania Bara imefikia tamati kwa kushuhudia timu za Ruvu Shooting na Polisi Morogoro zikiipa mkono wa kwa heri ligi hiyo.

Matokeo ya mechi zote za leo yako kama ifuatavyo:
Azam FC 0-0 JKT Mgambo
JKT Ruvu Stars 1-2 Simba SC
Kagera Sugar 0-0 Tanzania Prisons
Mbeya City 1-0 Polisi Morogoro
Mtibwa Sugar 1-2 Coastal Union
Ndanda FC 1-0 Young Africans
Stand United 1-0 Ruvu Shooting


Kwa matokeo hayo, Ruvu shooting imebaki na pointi zake 29 huku Mgambo nayo ikifikisha pointi 29 sawa na Prisons iliyomaliza pia ikiwa na pointi hizo hizo 29 lakini Prisons na Mgambo zikiipiku Ruvu shooting kwa tofauti ya magoli.

Kwa upande wa Polisi Moro yenyewe iliendelea kubaki na pointi zake 25 baada ya kupoteza mchezo wa leo dhidi ya Mbeya City.

Hivyo timu 2 za mwisho katika msimamo wa ligi hiyo ni Polisi na Ruvu Shooting, wakati Stand, Mgambo, Ndanda na Prisons zikijinasua baada ya matokeo ya leo.
Angalia vizuri hapa chini

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post