DC MAKONDA AFUNGUKA KUHUSU MGOMO WA MADEREVA NA ISHU YA KUPIGWA MAWE!!




Vichwa vya habari magazetini, kwenye radio na TV kwa siku mbili mfululizo ilikuwa ishu ya mgomo wa madereva wa mabasi ya abiria.. jana mchana Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akafika kituo cha Mabasi Ubungo akaongea na madereva na kuwaahidi kushughulikia hii ishu, mgomo ukaisha safari za mabasi zikaendelea kama kawaida.


Leo kaja na majibu kuhusu kile ambacho Serikali imeamua kuhusu kushughulikia kero mbalimbali za madereva zilizofanya wakafanya mgomo; >>

Tumekaa jana na ahadi yangu imetimia.. niliahidi ya kwamba kama kile kikao hakitakuwa na majibu ambayo ndugu zangu madereva wanayataka mimi nitatangaza mgomo leo, lakini jana nimekutana na Waziri wa Uchukuzi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri wa Kazi, Naibu Waziri wa Fedha, SUMATRA, TABOA , TATOA na Afande Mpinga.. Chini ya Waziri Mkuu wameunda Kamati ambayo itashughulika na kero zote za usafiri na ni Kamati ya Kudumu>>– DC Paul Makonda.

>>Madereva watakua na watu watano wa kuwawakilisha kwenye hicho.. nina uhakika kwamba chombo hiki kitajibu kero zao.. Kamati hii ni ya kudumu kwa kuwa hatujui kesho kuna kero gani itatokea.. lengo ni kutatua changamoto zote za usafiri nchini kwa muda wote badala ya kusubiri mgomo utokee ndiyo tuanze kutafuta majibu>>– DC Makonda.

“Watu wengi hawapendi watu wasiowapenda wafanye mambo mazuri.. Mkuu wa Wilaya kama alipigwa mawe basi Mkuu wa Wilaya huyu Makonda ni mkubwa kuliko hata mawe, waliokuwa wakimpiga mawe walikubali vipi kumsikiliza wakaweka mawe pembeni.. mimi sikupigwa mawe“>>–DC Paul Makonda.

Majibu hayo ya Paul Makonda utayasikia pia kwenye hii sauti hapa, bonyeza play

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post