AUAWA KWA KUNYONGWA NA MME WAKE BAADA YA KULEWA POMBE ZA KIENYEJI KISA WIVU WA KIMAPENZI HUKO KAHAMA


Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Prisca Pinzure(40), mkazi wa kijiji cha Bulima kata ya Mwaluguru wilayani Kahama mkoani Shinyanga ameuawa kwa kunyongwa shingo chumbani kwa na mume wake baada ya kulewa pombe za kienyeji kutokana na wivu wa kimapenzi.


Kamanda  wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha amesema tukio hilo limetokea Mei 4 majira ya saa moja asubuhi mwaka huu.Amesema kabla ya mauaji hayo Mei 3  mwaka huu,muda wa jioni marehemu alikuwa na mume wake Isaya Kuzenza (40), kwenye klabu za pombe za kienyeji wakinywa pombe hizo.


Kamanda Kamugisha amesema chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi ambapo wanandoa hao, walikuwa na tabia ya kugombana kila wanapokunywa pombe hizo za kienyeji.


Tayari jeshi la polisi  linamshikilia mme wa marehemu kwa uchunguzi zaidi juu ya mauaji hayo.

Na Marco Maduhu-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post