Taarifa Muhimu!! KUHUSU AJIRA MPYA ZA WALIMU WA SEKONDARI MWAKA 2014/2015


TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUONDOLEWA ORODHA YA WALIMU WA MASOMO YA SANAA NA BIASHARA WA SHULE SEKONDARI -AJIRA MPYA MWAKA 2014/15

Orodha ya wahitimu wa shahada na stashahada waliopangiwa katika halmashauri mbalimbali inafanyiwa marekebisho baada ya kubainika kuwa uongozi wa Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa (Sebastian Kolowa University College-SEKUCO) cha Lushoto uliwasilisha orodha ya wahitimu wapatao 491 wa mwaka 2013 ambao walishaajiriwa badala ya wahitimu wa mwaka 2014.

Kutokana na sababu hiyo, orodha tajwa imesitishwa kwa muda ili kufanyiwa marekebisho na kuwekwa orodha sahihi itakayojumuisha wahitimu wa SEKUCO wa mwaka 2014.
Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kutokana na kasoro hiyo.

Imetolewa na
OFISI YA WAZIRI MKUU - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI

Chanzo-EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527