ANGALIA PICHA_KIKAO CHA UHAMASISHAJI WA MASUALA YA LISHE KWA VIONGOZI WA MKOA NA WILAYA SHINYANGA
Thursday, April 23, 2015
Taasisi ya Chakula na Lishe nchini kwa kushirikiana na ofisi ya mganga mkuu mkoa wa Shinyanga jana
Aprili 22,2015 wamefanya kikao cha Uhamasishaji wa Masuala ya Lishe kwa
viongozi wa mkoa wa Wilaya iliyofanyika katika ukumbi wa Empire Mult Hotel
mjini Shinyanga-Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga
Lengo la kikao hicho ni kuwapatia viongozi hamasa katika
kupambana na matatizo ya Lishe Duni inayoathiri afya na maendeleo katika mkoa
ikiwa ni pamoja na wanafunzi kutofanya vizuri darasani na kuongeza maradhi na
vifo hasa kwa watoto wa umri chini ya miaka mitano na wanawake walio katika
umri wa kuzaa.
Kulia
ni Mkurugenzi wa taasisi ya Chakula na Lishe nchini Tanzania Dr Joyceline
Kaganda akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema takwimu za lishe mkoa wa
Shinyanga mwa ka 2014 zinaonesha kuwa asilimia 30 ya watoto wamedumaa ukilinganisha
na mwaka 2010 ambapo asilimia 43 ya watoto walikuwa wamedumaa huku wilaya ya
Kishapu ikiongoza ikifuatiwa na wilaya ya Shinyanga,Ushetu,Msalala,Shinyanga
manispaa na Kahama mji.Kushoto kwake ni kaimu mganga mkuu mkoa wa Shinyanga Dr
Fabian Kalabwe kwa niaba ya katibu tawala mkoa wa Shinyanga.
Wajumbe wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea kwenye kikao
Mkurugenzi wa taasisi ya Chakula na Lishe nchini Tanzania Dr Joyceline Kaganda akizungumza katika kikao hicho
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini
Kaimu
mganga mkuu mkoa wa Shinyanga Dr Fabian Kalabwe kwa niaba ya katibu tawala mkoa
wa Shinyanga akitoa hotuba ambapo alizitaka halmashauri za wilaya na mkoa
kujumisha shughuli za lishe na kupewa kipaumbele katika mipango yao huku
akizitaka halmashauri ambazo bado zinatumia waratibu wa lishe wasio na sifa
waache mara moja kwani watakosa fursa nyingi hasa miradi inayosimamiwa na
wahisani.
Mwezeshaji
wa kitaifa kwa viongozi ngazi za mikoa na wilaya ambaye pia ni Afisa Lishe mkoa
wa Iringa Mwita Waibe akitoa mada ambapo alisema miongoni mwa nchi zinaongoza
kwa utapiamlo barani Afrika ya Kwanza ni Ethiopia,ya pili DRC,Tanzania
inachukua nafasi ya tatu.
Kikao kinaendelea
Mwezeshaji wa kitaifa kwa viongozi ngazi za mikoa na wilaya ambaye pia ni Afisa Lishe mkoa wa Iringa Mwita Waibe alitaka elimu itolewe kwa wananchi juu ya umuhimu wa lishe kwa watoto ndani ya siku 1000 ili kuwaepusha na udumavu.Alisema katika mkoa wa Shinyanga kati ya watoto 100,30 wamedumaa hivyo kuitaka jamii kuwapa watoto vyakula vyenye madini joto ili kujenga ubongo wao-Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin