Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TAZAMA PICHA_KILICHOJIRI KWENYE KIKAO MAALUM CHA KUNUSURU SHIRECU SHINYANGA

Hapa ni katika ukumbi wa mikutano katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga ambapo jana Aprili 22,2015 kumefanyika kikao maalum mjini Shinyanga  kilichoshirikisha viongozi  wa serikali wa mikoa na wilaya kutoka mkoa wa Simiyu na Shinyanga kikilenga   kukinusuru Chama  Kikuu cha Ushirika mkoa wa Shinyanga(SHIRECU)  kutokana na changamoto zilizopo za  ushindani wa kibiashara kwenye zao la pamba ambalo ni tegemeo kwa mikoa ya kanda ya ziwa.Kikao hicho kilihudhuriwa na wakuu wa mikoa ya Shinyanga na Simiyu,wakuu wa wilaya,wakurugenzi wa halmashauri za wilaya na miji na watendaji mbalimbali wa serikali-picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga
Mwenyekiti wa SHIRECU Robert Seleman Mayangela akifungua kikao hicho ambapo alisema hicho ni kikao cha kazi na utekelezaji ili kukabiliana na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo.

Wajumbe wa kikao wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
 Mkuu wa mkoa wa Shinyanga  Ally Rufunga akitoa hotuba yake ambapo pamoja na mambo mengine aliitaka SHIRECU kuviendeleza vyama vya ushirika ambavyo vinasuasua ,huku akiwatahadharisha viongozi wa serikali na wanasiasa kuwa hawaruhusiwi kuwa viongozi ndani ya vyama vya ushirika ili kuepusha migongano ya kimaslahi.
Wakuu wa wilaya wakiwa ukumbini
Meneja mkuu wa SHIRECU mkoa wa Shinyanga Joseph Mihangwa akitoa taarifa ya shughuli za SHIRECU 1984 Limited ambapo alisema hadi kufikia Mwezi Machi 2015 ina vyama vya Ushirika vya Msingi wanachama hai 500 na vyama sinzia ( ambavyo havina kazi) 250

Meneja mkuu wa Shirecu mkoa wa Shinyanga Joseph  Mihangwa alisema hadi kufikia Desemba mwaka 2014  walikuwa na rasilimali zisizoondosheka zenye thamani ya shilingi 47 bilioni ambazo zinapaswa kuendelezwa na kuboreshwa vikiwemo viwanda  vya kuchambua pamba na kusindika mafuta.


 Mihangwa alisema katika msimu huu wa 2015/2016 wamejipanga kununua kilo milioni 15 za pamba katika mkoa wa Shinyanga,Simiyu na Geita kwani uwezo wa pesa upo.
Meza kuuu wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini

Kikao kinaendelea


Kikao kinaendelea ambapo wajumbe wa kikao hicho waliitaka Shirecu kuangalia uwezekano wa kuanza kuongeza thamani kwenye zao la pamba ili kupata faida zaidi na kuachana na mfumo wa kizamani wa kuuza pamba tu-picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com