
Jeshi la Polisi mkoani Singida, linamshikilia Jumanne Yusuph (33),
Mkazi wa Kijiji cha Mtamaa ‘A’ Manispaa ya Singida kwa kumuua mama yake
mzazi, Tausi Abdalah (56) kwa kumchinja na kisu shingoni, juzi alfajiri
katika kijiji hicho.
Baada ya kumchinja mama yake, kijana huyu alikwenda
kwa mama yake mkubwa kutoa tarifa, kisha tena akaenda kwa mwenyekiti wa
kijiji kumjulisha kuwa amefanya mauaji ya mama yake.
Kabla ya
mauaji hayo, mtuhumiwa huyo aliwaua ng’ombe watatu wa mama yake kwa
kuwacharanga na mapanga.
Pia inadaiwa kuwa aprili 16 mwaka huu, mtuhumiwa
huyo alifika kwa mama yake na kubomoa sehemu ya nyumba yake kisha
akatokomea kusikojulikana.
Social Plugin