ANGALIA PICHA- KOLANDOTO FC WAIBUKA WASHINDI MASHISHANGA CUP,WAONDOKA NA ZAWADI KIBAO


Kulia ni mbunge wa Viti maalum mkoa wa Shinyanga(CHADEMA) Rachel Mashishanga akisalimiana na mwenyekiti wa shirikisho la mpira wa miguu wilaya ya Shinyanga mjini (SHIDEFA) Salum Kitumbo wakati wa fainali ya ligi ya Mashishanga Cup katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga,ambapo timu zilizofika fainali ni timu ya Kolandoto FC na Veterani FC .
Ligi hiyo ilikuwa inashirikisha timu za mpira wa miguu na pete kutoka kata 17 za manispaa ya Shinyanga yaliyoanza Januari 8 mwaka huu na kumalizika Februari 25,2015.
 
Lengo la  mashindano hayo ni kuinua vipaji vya mpira na kuinua soka katika manispaa ya Shinyanga, mashindano ambayo yalifadhiliwa na mbunge huyo-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Shinyanga

 
Wakazi wa Shinyanga wakiwa katika viwanja vya Shycom Mjini Shinyanga kushuhudia mchezo wa fainali kati ya Kolandoto Fc na Veterani fc katika mashindano ya Mashishanga cup yaliyofadhiliwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Rachel Mashishanga-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Shinyanga
Kapteni wa Timu ya mpira wa miguu ya kata ya Kolandoto Juma Tunze akimtambulisha mbunge Rachel Mashishanga kwa wachezaji wa timu hiyo kabla ya mchezo wa fainali kati yake na Veteran fc ya Kata ya Shinyanga mjini-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Shinyanga

Mheshimiwa Mashishanga akisalimiana na wachezaji wa timu ya Veteran fc ( aliyemshika mkono ni aliyekuwa kocha wa timu ya Stand United Emmanuel Massawe)-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Shinyanga

Mbunge akiendelea kusalimiana na wachezaji na kuwatakia mchezo wenye amani na utulivu-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Shinyanga


Jukwaa kuuu wakishuhudia mpambano huo,wa kwanza kushoto aliyevaa suti ni askofu wa Kanisa la Emmanuel mjini Shinyanga Edson Mwombeki-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Shinyanga
 
 Mchezo kati ya Vetereani fc(jezi nyeupe) na  Kolandoto ukiendelea ambapo
katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo timu ya kolandoto ilipata magori mawili kupitia kwa wachezaji wake ,Juma Tunze ambaye alifunga dakika ya 25, na gori la pili lilifungwa na Jacob Faustine dakika 43, kwa njia ya penati-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Shinyanga

Hata hivyo katika kipindi cha pili kikiendelea dakika ya 53, timu ya Veterani ilipata gori la kwanza la kufutia machozi kupitia kwa mchezaji wake Portion Mtware, ambapo dakika ya 78, Juma Tunze akaiongezea timu yake ya Kolandoto bao la tatu, pamoja na Doto James akaongeza bao la nne dakika ya 84-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Shinyanga
 
 Mchezo unaendelea-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Shinyanga

MC Maarufu mjini Shinyanga ICE akifanya yake uwanjani wakati wa mchezo huo-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Shinyanga

Wananchi wakishuhudia mpambano- Baada ya mchezo huo mbunge Mashishanga ambaye ndiye mfadhili wa ligi hiyo, alitoa zawadi kwa mshindi wa kwanza ambaye ni kolandoto pesa taslimu shilingi laki tano pamoja na kikombe, huku mshindi wa pili vetereni akipewa laki tatu na mipira miwii pamoja seti moja ya jezi, ambapo mshindi wa tatu Ngokolo akipewa laki mbili na mipira mitatu-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Shinyanga

 Mchezo unaendelea-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Shinyanga
Mbwembwe uwanjani-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Shinyanga

 Mchezo unaendelea-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Shinyanga

Mshindi wa pili katika mpira wa miguu Veterani fc wakipokea zawadi ya shilingi laki 3,mipira miwili na seti moja ya jezi kutoka kwa mbunge huyo-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Shinyanga
Mheshimiwa Mashishanga akikabidhi kiatu cha uchezaji bora kwa mchezaji  Juma Tunze kutoka Kolandoto fc kiatu ambacho kinafananishwa na kiatu cha dhahabu-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Shinyanga

Mbunge akikabidhi kombe kwa mshindi wa kwanza katika mashindano hayo Kolandoto fc ambao mbali na kombe pia waliondoka na kitita cha shilingi laki 5-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post