NUH MZIWANDA AOMBA RADHI KWA PICHA YA UCHI ALIYOPIGA NA SHILOLE NA KUIWEKA MTANDAONI




Mwanamuziki Nuhu Mziwanda ambae ni mchumba wa mwanamuziki Shilole (Shishi baby) ameomba radhi jana kupitia ukurasa wake wa Intragram baada ya kupost picha ambayo inaonyesha maungo ya ndani ya mpenzi wake huyo walipokuwa wakioga,picha hiyo ilimuonyesha Shilole akiwa kifua wazi.Kwa mujibu wa Nuhu Mziwanda amesema kuwa alipost picha hiyo ili apate Kiki kwa ajiri ya video yake mpya ya Zimataa ambayo bado haijatoka mpaka.
Baada ya juzi usiku Nuhu mziwanda kupost picha hiyo kwenye ukurasa wake mashabiki zake walionyesha kutofurahishwa na kitendo hicho na wengihne kufikia hatua ya kutukana huku wengine wakidai kuwa amemdharirisha mpenzi wake huyo ambae ni mama wa watoto wawili.lakini baada ya hapo Nuhu aliifuta picha hiyo alipogundua hali ya upepo imekuwa tofauti na vile ambavyo yeye alidhania.
Anapenda mwenyewe kuzalilishwa huyo @shilolekiuno kwani ni picha yake ya kwanza???? ... nawapenda lakini wameniuziii toka wapost ule ujinga,na kujisahaulisha kama wee ni mama wa mabinti wakubwa tu sijui wanajifunza nini wakiona hizo picha..."Kapost mpenz wake yuko maziwa wazi yale sio mapenzi unaitwa uzalilishaji Wa wanawake Hao ni baadhi ya mashabiki waliotoa yao ya moyoni baada ya kuiona ile picha ya Nuhu wakiwa pamoja na Shilole.
"Naomba niombe radhi kwa waliochukizwa na picha niliopost usiku wa jana.Lakini naweza sema pia ile ilikuwa ni video yangu mpya ya wimbo wangu wa Zimataa.So ilikuwa ni promotion picture.Ila mwisho wa maneno yangu ni kuomba radhi kwa lililotokea."
Hata baada ya kuomba radhi hali ya mashabiki bado ilikuwa ileile ni watu walionyesha kukerwa na kitendo kile bado waliendelea kutukana na kusababisha hata post ya kuomba radhi pia kuifuta katika Account yake hiyo ya Instragram.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527