PICHA ZA MWANAFUNZI ALIYEVUNJWA MGUU VURUGU ZA UDOM ZINATISHA,HABARI KAMILI IKO HAPA


Mguu  wa kijana Iddy ukiwa katika hali mbaya



Mwanafunzi wa UDOM aliyejulikana kwa jina la Iddy aliyeuamia mguu

Mr Dannis akiwa na Msouth Kato baada ya kumtembelea kijana ambaye ni mwanafunzi wa Udom aliyepata majanga ya kuvunjika mguu baada ya kuruka kwenye gari na kutaka kuwakwepa Polisi waliokuwa wanahakikisha usalama unapatikana katika chuo hicho cha Udom kutokana na baadhi ya wanafunzi kuwashawishi wanzao kufanya maandamano yasiyokuwa ya Maani kutokana na kile kinachodaiwa kutopata Mkopo kwa muda unaostahili
Kijana ambaye ni mwanafunzi wa Udom anayefahamika kwa jina la Iddy aliyepata masaibu baada ya kuvunjika mguu katika vurugu za mgomo uliyofanywa na wanafunzi wa Udom wa college ya social science.. Kijana Iddy ambaye amelazwa katika hospitali ya General Dodoma leo hii amepatiwa msaada Mh Shabiby wa fedha za 
matibabu pamoja na while chair baada ya kuzuiliwa kutoka hospitali hapo kutokana na deni kubwa la matibabu aliyokuwa anadaiwa hospitalini hapo.. Paparazi wa blog ya Boss Ngasa alifanikiwa kupata nafasi ya kuongea na mzazi wa mwanafunzi huyo na kudai kuwa aliambiwa atapata msaada kutoka chuoni hapo lakini cha kushangza mpaka muda huu wa jioni hajapata msaada wowote kutoka chuo hicho zaidi ya kupigwa chenga na kutupiana mpira.. Baba wa kijana huyo ametoa shukrani za pekee kwa Mh Shabiby baada ya kuguswa kiubinadamu na kumsaidia kijana wake... Kijana Iddy kwa sasa anaendelea vizuri
TAARIFA YA POLISI IKO HAPA CHINI


Jeshi la polisi mkoani Dodoma limekanusha uvumi uliozagaa mitaani wa wanafunzi 2 kupoteza maisha huku wengine wanne wakijeruhiwa wakati wa maandamano ya wasomi wa ngazi ya Diploma wa kozi ya ualimu wa chuo kikuu cha Dodoma [UDOM].

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma David Misime amesema hakuna Mwanafunzi yeyote aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa wakati zoezi la kuwakamata wanafunzi hao waliokuwa wakiandamana kuelekea katika ofisi mbalimbali za serikali ikiwemo ya waziri mkuu.

Amesema ni kweli kuwa nguvu ya kutumia mabomu ilitumika wakati wa kuwakamata na wakati hali hiyo ikitokea wanafunzi hao walizagaa katika mitaa mbalimbali huku 84 kati yao wakikamatwa na kufikishwa mahakamani juzi asubuhi.

Kamanda Misime amesema kumekuwa na uvumi katika mitandao ya kijamii watu wanatumiana picha kwamba kuna wanafunzi wamefariki na wengine kujeruhiwa habari ambazo siyo za kweli.

Aidha Wanafunzi wa kozi ya ualimu ngazi ya Diploma waliandamana Januari 14 kwa lengo la kushinikiza uongozi wa chuo kuwapa fedha za mkopo unaotolewa na serikali ambapo kutokana na kukosa kunawafanya kuishi maisha magumu.


KUHUSU VINARA WA MGOMO KUFUKUZWA CHUO


Kufuatia Sakata la wanafunzi wa UDOM kugoma na kuandamana kwa ajili ya kudai stahiki zao mbalimbali ikiwemo mkopo Uongozi wa chuo hicho umewafukuza vinara 3 wa mgomo huo.

Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma [UDOM] Prof. Idris Kikula amesema kutokana na hali ya
wanachuo hao zaidi ya 2400 kuandamana pasipokufuata taratibu za kisheria za chuo na za nchi Bodi ya chuo imewafukuza 3 ambao ni viongozi katika kitivo cha Sayansi.

Makamu mkuu huyo wa chuo amesema waliofukuzwa ni Rais ,Waziri mkuu pamoja na katibu mkuu wa serikali ya wanafunzi katika kitivo cha Sayansi ambao ndiyo walikuwa vinara wa kuanzisha mgomo na kushawishi
maandamano.

Aidha amesema viongozi hao wa kitivo cha Sayansi walikuwa
wanawashawishi wenzao wakati wao hawapo katika Programu hiyo maalum.

Amebainisha kuwa wameshawakanya mara kadhaa lakini hawakusikia, sasa dawa yao ni hiyo pia bado wanaendelea na uchunguzi kubaini wote waliochochea maandamano hayo na watakaobainika sheria
itachukua mkondo wake.
Na Josephine Charles-Malunde1 blog Dodoma

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post