ASKARI WA JWTZ WAGONGWA GARI HUKO OLD SHINYANGA,MMOJA AFARIKI PAPO HAPO

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus KamugishaAskari wa jeshi la wananchi Tanzania MT.88596 Benard Mdika(29) wa kambi ya Old Shinyanga  amefariki dunia papo hapo baada ya pikipiki aliyokuwa akisafiria kugongwa na gari katika barabara ya Old Shinyanga maeneo ya shule ya sekondari KOM iliyopo katika kata ya  Lubaga manispaa ya Shinyanga.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha tukio hilo limetokea Januari 15,2015 saa 3:40 usiku baada ya gari lisilofahamika namba za usajili,dereva wala mmiliki wake liligonga pikipiki yenye namba za usajili T.984 BGH aina ya sunlg ikiendeshwa na askari huyo.

Kamanda Kamugisha alisema askari huyo kutoka kambi ya jeshi ya Old Shinyanga aliyekuwa anaendesha pikipiki hiyo alifariki dunia papo hapo huku abiria wake ambaye pia ni askari wa jeshi la wananchi MT 88789 PTE Nicholaus  Donald(29) mkazi wa Old Shinyanga akijehuhiwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake.

Kamanda huyo alisema  Nicholaus Donald  aliumia usoni na kichwani na amelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga na hali yake inaendelea vizuri.

Alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa gari na jeshi la polisi linaendelea na juhudi za kulitafuta gari husika na dereva.

Na Kadama Malunde-Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post