Saturday, December 27, 2014

Utamaduni Lake Zone_ SIMULIZI YA KUTISHA KUHUSU GAMBOSHI- SEHEMU YA MWISHO

  Unknown       Saturday, December 27, 2014
 Kama tulivyoawaahidi kuwaletea simulizi mbalimbali kuhusu kanda ya Ziwa Victoria,kupitia ukurasa/kipengele chetu kipya cha" UTAMADUNI LAKE ZONE",angalia juu kwenye blog,kila siku za Jumamosi ,leo Malunde1 blog inakuletea sehemu ya MWISHO  ya simulizi ya kusisimua kuhusu Gamboshi


SIMULIZI YA KUSISIMUA KUHUSU GAMBOSHI SEHEMU YA MWISHO LEO

Ilipoishia...........


Hatua niliyokuwa nimeipanga ni kuonana naye uso kwa uso, ilikuwa mishale ya asubuhi nilijiandaa vya kutosha kwa ajili ya kuonana na MCHUNGAJI.

Nikiwa na mkoba wangu nilienda moja kwa moja kwenye ofisi ya MCHUNGAJI.

Kabla hujafika kwenye ofisi ya MCHUNGAJI lazima upite mapokezi kwanza.


Basi nilimkuta dada mmoja na kumuuliza kama MCHUNGAJI nimemkuta.


Aliniambia yupo na kuniuliza nina ahadi naye? Nilimjibu hapana.


Alichukua simu ya mezani kumpigia MCHUNGAJI, MCHUNGAJI alisema tuende wote ofisini kwake maana mimi nilikuwa mgeni.

Tulipoingia ofisini kwa MCHUNGAJI, MCHUNGAJI alisimama ghafla kutoka kwenye kiti alichokuwa amekalia na kuita jina Neema!!!!!!! Neema !!!!, 


Dada wa mapokezi aliniuliza unaitwa Neema??? Nilimjibu hapana! Na MCHUNGAJI aliduwaa sana mpaka akaanguka chini akazimia.
Endelea ..............

Pia na sisi tukiwa katika hali ya stofahamu tulibaki tukishangaa kilichomkuta mchungaji, Dada alitoka nje kumuita mwinjilisti aliyekuwa ofisi tofauti na ya mchungaji.

Dada alipotoka nje, nilibaki mimi na mchungaji ambaye alikuwa amepoteza fahamu, nilijifikiria kuwa huu ni muda mwafaka wa kuweza kufanya kazi iliyonileta, haraka haraka nilifungua mkoba wangu na kuchukua baadhi ya dawa tunazotumia kwa ajili ya kupoteza uhai wa mtu.

 Juu ya meza yake kulikuwa na glass niliichukua nikamimina maji ndani yake na dawa nikatia ndani.

Glass iliyo na maji pamoja na dawa niliichukua na kuelekea kwa mchungaji ili kumnywesha.

 Glass nilipoisogeza karibu na mdomo, sauti ilisikika ikisema "mwanangu sijakuleta Duniani kwa kazi hiyo!

Nilista kidogo tena kwa mshangao kimoyomoyo nilijisemea "potelea mbali liwalo na liwe!".

Kwa mara ya pili nilishika glass lakini kiliposogeza mdomoni mwa mchungaji, mkono wangu na mwili sehemu zote nilihisi kama nimepigwa na shoti ya umeme na nguvu niliishiwa na  kupoteza fahamu.

Baada ya muda nilipata fahamu nikiwa ndani ya kanisa nikiwa nimezungukwa na watu wengi sana pia nikiwa nimerudia jinsia yangu ya kiume na nywele zangu ndefu kupita kiasi.

Nikiwa na akili zangu timamu, mchungaji aliniuliza unaitwa nani? Nilimjibu naitwa Timothy mchungaji aliniita Timoth niliweza kuitika.

 Kipindi hicho chote nilikuwa kama nilivyozaliwa lakini wasamalia wema walinipa nguo zao na kuweza kujifunika sehemu zinazohusuka.

Mchungaji alinichukua na kunipeleka mpaka nyumbani kwake.

 Mchungaji aliniuliza kijana vipi unajisikiaje? Nilimjibu najisikia vizuri (tulikuwa tunaongea kwa kiingereza).

 Nilimwambia mchungaji unakumbuka siku uliyotekwa ndani ya boti na wenzio wote walikufa ??

 Mchungaji alionekana kushituka kidogo kwa mshangao!

 Na kusema " ndiyo nakumbuka sana" mchungaji alinikatiza kidogo na kuniambia twende kanisani ukatoe kama ushuhuda ili na wengine waweze kuokoka kupitia kwako.

Kanisa lilikuwa na watu wengi sana niliwekwa mbele ya waumini niweze kutoa ushuhuda, kwa kweli nilijiamini sana nilianza kwa jina na nchi niliyotoka pamoja na maisha niliyoyapitia kuanzia GAMBOSHI sehemu ya kwanza hadi hapa yote niliieleza kama ushuhuda, pia na sababu iliyopelekea kumuua mchungaji nilieleza kama nilivyoeleza tangu mwanzo.

Mchungaji alininunulia nguo mpya na kunipeleka saluni, alipomaliza hayo yote alinipeleka katika ubalozi wa Tanzania aliwaeleza yote yaliyojili pia na mimi waliniita na kunihoji baadhi ya maswali kutoka Tanzania na niliyajibu kwa ufasaha, walipo maliza kunihoji walitukabidhi tiketi ya ndege kurudi Tanzania.

Nilipofika nyumbani kila mtu alikuwa ananikimbia na kusema una miaka minne na nusu umekufa leo iweje urudi tena ukiwa hai?

Walinilazimisha kunipeleka kwa waganga wa kienyeji lakini nikikataa na kuwaambia namwamini mungu wangu ndiyo maana kanifanya niwe hapa!

Siku ya Jumapili nilienda kanisani kutoa ushuhuda, watu wengi sana waliokoka na kuamini kuwa mungu yupo.

Kazi yangu kwa sasa ni kueneza injili.

Mhubiri 12:1....
Asanteni wote waliokuwa na mimi tangu mwanzo wa stori hii na mungu awabariki sana.
Karibuni Shinyanga
Kheri ya mwaka mpya.

Mpenzi msomaji wetu wa Malunde1 blog simulizi ya Gamboshi ndiyo imefika mwisho kumbuka tu kwamba simulizi hii ilikuwa inaletwa kwenu na ndugu Timoth Mathias (pichani) anapatikana kwa simu namba 0764676242
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post