Baadhi ya wananchi wa kitongoji cha Bulima , kijiji cha Bulima kata ya Mwamanyili wilaya ya Busega mkoani Simiyu wakisubiri kupiga kura asubuhi hii-picha na Damian Lupimo Kageba
SAA 11.45 AM
Simiyu: Habari kutoka katika kata ya Mwamanyili katika wilaya ya Busega mkoani Simiyu zoezi la kupiga kura bado halijaanza,tunaambiwa majina ya wagombea hayaonekani,yaliyopo ni wajumbe pekee~Damian Kageba
Kagera:Wagombea wa CCM katika mitaa 3 ya kata ya Kibeta Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wamejiuzuru asubuhi ya leo na kuwaacha wagombea wa uenyeviti wa Chadema kupita bila kupingwa, na masunduku ya kura kurejeshwa kwa msimamizi mkuu wa uchaguzi~Essau Ezra
Rukwa:Mpaka sasa hawajaanza kupiga kura katika manispaa ya Sumbawanga mkurugenzi hapatikani na kuna fujo za hapa na pale, wanasema hakuna kituo hata kimoja wanachopiga kura~Luteja Abel
Shinyanga:EBANA ISAKA WILAYANI MPAKA SASA SAA TANO HATUJAPIGA KURA~Agustino John
Mwanza: Hatujaanza kupiga kura hadi sasa vifaa havijaja huku wilaya Sengerema kata ya Bulyaheke kijiji cha Kanyala zamani ilijulikana Lushamba~Khamis Kisimiza
Mbeya:Dah!!Sisi waandishi wa habari tunapata shida sana leo asubuhi nilienda kutembelea vituo vya kupigia kula hapa Mbeya kituo changu cha kwanza kilikuwa eneo moja linaitwa IGODIMA SHULE YA MSINGI pale nimemkuta mwanahabari mwenzagu Sadiki Nassoro ambaye pia ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi pale Ilemi Polythechnic College kilichompata inauma sana yeye alikuwa anapiga picha lakini wananchi wamempiga na kumrushia maneno makali huku wakishinikiza kwa polisi picha alizopiga zifutwe maana yeye ni mtu wa UVCCM habari ambazo ni haikuwa rahisi kuzifahamu kwa wakati ule.Halafu kibaya zaidi wananchi waliojitokeza ni zaidi ya 300 na polisi waliopo ni wawili tu,Je tume ya uchaguzi hawakujiandaa~Mathew Malunde
NGARA:Kutoka wilaya ya Ngara ni kwamba vituo vya Kichacha, Mumilango, Djuruligwa na Kanazi wilayani Ngara mkoani kagera ni kwamba Vituo bado havijafunguliwa licha ya kuwa tayari ni saa tatu dakika 43 na wananchi wanasubiri kupiga kura.
Dar es salaam:Wilaya Ilala kata Segerea mtaa wa Amani mkoa Daresalaam hatujaanza kupiga kura~Veronica Joram
Kagunga, Kigoma Kaskazini: Uchaguzi katika Vijiji vya Zashe na Kagunga, Kata ya Kagunga, Jimbo la Kigoma Kaskazini umefutwa hadi itakapotajwa tena baada ya Mtendaji wa Kata kuwaengua ACT katika uchaguzi huo baada ya kudaiwa kuwa wagombea wawili wa vijiji hivyo kutoka ACT walitumia anuani ya shule kama anuani yao. Hata hivyo Msimamizi Mkuu amesema anafuta uchaguzi hadi watakapotangaza tena.
SAA 13.36PM
KISHAPU: kama uko karibu saa hiv njoo kata ya Itilima ujionee majanga ya uchaguzi kalatasi za kupigia kura ndo zimefika kalam hamna mkuu wa wilaya Kishapu na mkuu wa pols Kishapu wamesema mwisho wa kupiga kura ni saa 3 usiku~Emmanuel Masanja
SAA 15:00PM
TANGA: Vituo 13 vimeahirisha uchaguzi hadi Jumapili wiki ijayo kwa sababu mbalimbali
KISHAPU: Even Kishapu baadhi ya sehemu hawajaanza mpaka saiv saa tisa kisa karatasi za kupigia hakna hadi huruma raia wanavyotapatapa hapa kituo cha kupigia hapa kijijini MWAJIGINYA,UKENYENGE!~Samson Peter Duttu
SENGEREMA:Uchaguzi huku wilaya Sengerema kata ya Bulyaheke kijiji cha Kanyala zamani ilijulikana Lushamba umeahirishwa mpaka wiki ijayo kisa masanduku hayafika na karatasi ni maajabu haya~Khamis Kisimiza
Dar es salaam:Wilaya Ilala kata Segerea mtaa wa Amani mkoa Daresalaam hatujaanza kupiga kura~Veronica Joram
SAA 12:00PM
SIMIYU_Wagombea wajiondoa baada ya kutishiwa kuuawa>>soma hapa>>KUUAWA
Shariff Shamba, Ilala: Eneo la Shariff Shamba, Ilala jijini Dar uchaguzi umeahirishwa mpaka Jumapili ijayo baada ya vifaa kutopatikana ndani ya muda muafaka. Vyama vyote vinavyoshiriki vimeafikiana.
Kagunga, Kigoma Kaskazini: Uchaguzi katika Vijiji vya Zashe na Kagunga, Kata ya Kagunga, Jimbo la Kigoma Kaskazini umefutwa hadi itakapotajwa tena baada ya Mtendaji wa Kata kuwaengua ACT katika uchaguzi huo baada ya kudaiwa kuwa wagombea wawili wa vijiji hivyo kutoka ACT walitumia anuani ya shule kama anuani yao. Hata hivyo Msimamizi Mkuu amesema anafuta uchaguzi hadi watakapotangaza tena.
SAA 13.36PM
KISHAPU: kama uko karibu saa hiv njoo kata ya Itilima ujionee majanga ya uchaguzi kalatasi za kupigia kura ndo zimefika kalam hamna mkuu wa wilaya Kishapu na mkuu wa pols Kishapu wamesema mwisho wa kupiga kura ni saa 3 usiku~Emmanuel Masanja
SAA 15:00PM
TANGA: Vituo 13 vimeahirisha uchaguzi hadi Jumapili wiki ijayo kwa sababu mbalimbali
KISHAPU: Even Kishapu baadhi ya sehemu hawajaanza mpaka saiv saa tisa kisa karatasi za kupigia hakna hadi huruma raia wanavyotapatapa hapa kituo cha kupigia hapa kijijini MWAJIGINYA,UKENYENGE!~Samson Peter Duttu
SENGEREMA:Uchaguzi huku wilaya Sengerema kata ya Bulyaheke kijiji cha Kanyala zamani ilijulikana Lushamba umeahirishwa mpaka wiki ijayo kisa masanduku hayafika na karatasi ni maajabu haya~Khamis Kisimiza
Mtandao Huu Unakujali,Ni Wako!! Tunataka Tukutumie Habari zetu Zote Mara Tu Tunapozipandisha Mtandaoni.Kujiunga nasi Bonyeza Hapa Sasa Hivi ><<VITUKO>>,"MAPENZI",<<HABARI MSETO>>MAGAZETI

Social Plugin