ASKOFU MWOMBEKI AITANGAZIA VITA CCM-AJITOA MHANGA KUIPIGIA DEBE CHADEMA JIMBO LA KISHAPU NA SHINYANGA MJINI


Askofu wa Kanisa la TFE  la mjini Shinyanga, Edson Mwombeki
Askofu wa Kanisa la Tanzania Field Evangelism(TFE) maarufu kanisa la Emmanuel la mjini Shinyanga, Edson Mwombeki, amesema atakipigia ‘debe’ Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika uchaguzi mkuu ujao.

Askofu Mwombeki alitoa ahadi hiyo  mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Shinyanga wakati akiwaweka wakfu viongozi wapya wa Chadema walioshinda katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji mbele ya Mbunge wa Viti Maalum Shinyanga Mjini, Rachel Mashishanga.

Alisema maono aliyoyapata, chama hicho kitakuwa mkombozi kwa Watanzania katika kuwaletea maendeleo na si chama kingine, hivyo atahakikisha anakuwa mstari wa mbele kinapata ushindi katika majimbo ya Kishapu na Shinyanga Mjini.

“Magari yangu mawili yatatumika kufanya kampeni kwa gharama zangu katika majimbo haya kutokana na kutokuwa na viongozi wazuri na kutozingatia maslahi ya wananchi,” alisema Mwombeki.

Aidha, alisema CCM iliyoachwa na hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, siyo CCM ya sasa kwani haina sera nzuri, viongozi wabovu ambao hawafuati sera ya chama hicho na badala yake wanafuata mambo yao binafsi.

"Viongozi hasa wabunge waliochaguliwa na wananchi hawako karibu na viongozi wa dini na  wananchi wao,hii ni kero kubwa,wabunge  badala ya kuwa karibu na wananchi wao  sasa wamekuwa walanguzi wa  wananchi",alisema Askofu Mwombeki

"Wakati wa uchaguzi wamekuwa wakijidai kutumia pesa zao na kupenda kuwarubuni wananchi katika jamii na walioko makanisani ,hii ni kero,vitendo vyao haviridhishi  mfano mbunge anapodiriki kwenda kununua viwanja vya kanisa na kuvifanya kuwa gereji",aliongeza Mwombeki.

 Na Mwandishi wa Malunde1 blog-Shinyanga 

Bonyeza hapa Tukupe habari zote mara moja zikitoka "HABARI" VITUKO "MAPENZI"MAGAZETI,UDAKU>
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527