ANGALIA PICHA- JINSI WATOTO WENYE ULEMAVU WALIVYOUAGA MWAKA 2014 NA KUUKARIBISHA MWAKA 2015 SHINYANGA

Watoto wenye ulemavu wa ngozi(Albino),watoto wasioona na wasiosikia wanaolelewa katika kituo cha Buhangija Jumuishi katika manispaa ya Shinyanga wakiwasili katika kiwanda maarufu  cha Chakula cha Musoma Food mjini kwa ajili ya kula chakula kilichoandaliwa na uongozi wa kiwanda hicho lengo likiwa ni kuuaga mwaka 2014 na kukaribisha mwaka 2015 ikiwa ni utaratibu ambao kiwanda hicho kimejiwekea kuwa karibu na watoto hao ambao wanaonekana kutengwa na jamii-picha na Shaaban Alley-Shinyanga


Mkurugenzi wa kiwanda cha Musoma Food bwana Said Makiragi maarufu kwa jina la Musoma Food akiwapokea watoto hao baada ya kuwasili katika kiwanda chake-picha na Shaaban Alley-Shinyanga

  Mkurugenzi wa kiwanda cha Musoma Food bwana Said Makiragi akimshusha mmoja wa watoto hao kutoka kwenye gari baada ya kuwasili katika kiwanda hicho
-picha na Shaaban Alley-Shinyanga

Kulia ni mkurugenzi wa kiwanda cha Musoma Food  bwana Said Makiragi ambapo
alisema walemavu wa ngozi ni binadamu kama walivyo wengine na kwamba jamii inatakiwa kuachana na imani potofu za ushirikina kuwa viungo vya Albino vinasaidia kupata utajiri na kwamba utajiri unatokana na juhudi za mtu wala sio ushirikina -picha na Shaaban Alley-Shinyanga

Nje ya kiwanda cha Musoma Food kabla watoto hawajaanza kula chakula.Kushoto ni Mama Mkurugenzi wa Musoma Food-picha na Shaaban Alley-Shinyanga
Hapa ni nje ya kiwanda cha Chakula Musoma Food,watoto wenye ulemavu wa ngozi,wasiosikia na wasioona wakichukua chakula cha pamoja kuuaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka 2015 chakula kilichoandaliwa na
mkurugenzi wa kiwanda cha Musoma Food bwana Said Makiragi
-picha na Shaaban Alley-Shinyanga
Mkurugenzi wa kiwanda cha Musoma Food bwana Said Makiragi akigawa maji ya kunywa kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi,ambapo alitoa wito
kwa watanzania kutowatenga walemavu wa ngozi badala yake wawe karibu nao kwa kuhakikisha wanakuwa salama
-picha na Shaaban Alley-Shinyanga


Watoto wakiendelea kula chakula
-picha na Shaaban Alley-Shinyanga

Mkurugenzi wa kiwanda cha Musoma Food bwana Said Makiragi  akigawa maji kwa  watoto hao-picha na Shaaban Alley-Shinyanga

Watoto wakila chakula
-picha na Shaaban Alley-Shinyanga

Watoto wakiendelea kula chakula
-picha na Shaaban Alley-Shinyanga

Mkurugenzi wa Shalleyhabari blog ndugu Shaaban Alley akiwa na mtoto Kabula ambaye alikatwa mkono wake wa kulia na watu wasiojulikana kutokana na imani za kishirikina

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527