TAARIFA ZAIDI KUHUSU HELIKOPTA ILIYOUA WATU WANNE LEO JIJINI DAR ES SALAAM,TAZAMA PICHA HAPA

 Sehemu ya mabaki ya Helikopta baada ya kuanguka Ajali ya Helicopter ambayo imedaiwa kuwa ni mali ya Maliasili na Utalii imegharimu maisha ya marubani 3 wa Jeshi la Polisi Tanzania. Sp Kidai Kaluse, Insp.Simba Must Simba, Pc. Josso Selestine, Na rubani mmoja Capt. Khalfan,Ajali  hiyo imetokea huko Kipunguni B Moshi Bar,Ukonga-Ilala jijini Dar es Salaam. Chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana mpaka sasa. 
 Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova 
akifafanua jambo mbele ya Vyombo vya habari katika eneo la ajali,kufuatia kutokea kwa ajali hiyo iliyopelekea vifo vya watu wanne.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaa,Mh.Sadick Meck Sadick akizungumza mbele ya Vyombo vya habari katika eneo la ajali,kufuatia kutokea kwa ajali hiyo iliyopelekea vifo vya watu wanne
 Baadhi ya Wataalamu wakifanya uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo ya Helikopta.
 Baadhi ya watu wakishuhudia mabaki ya helikopta hiyo iliyopata ajali maeneo ya Kipunguni B Moshi Bar,Ilala jijini Dar es Salaam. 

BONYEZA HAPA UJIUNGE NASI TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA TU TUNAPOZIWEKA 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527