BUNGE LA TANZANIA LAAHIRISHWA HADI JANUARI 27,2015,WAHUSIKA WA ESCROW KUWAJIBISHWA

BONYEZA HAPA UJIUNGE NASI TUKUTUMIE HABARI ZETU MARA TU TUNAPOZIWEKA 


Bunge limeazimia waziri wa nishati na madini Mhe.Prof Sospeter Mhongo,Waziri wa ardhi Prof. Anna Tibaijuka,Mwanasheria mkuu wa serikali jaji Fredrick Werema na katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini pamoja na bodi ya wakurugenzi wa Tanesco wawajibishwe kwa kuishauri mamlaka ya uteuzi  kutengua uteuzi wao.

Akiwasilisha maazimio hayo mwenyekiti wa PAC Mhe. Zitto Kabwe amesema bunge pia linapendekeza serikali kuangalia uwezekano wa kuinunua mitambo ya IPTL na kuikabidhi kwa Tanesco,pamoja kamati za kudumu za bunge zichukue hatua za haraka kabla ya mkutano wa 18 wa kuwavua nyazifa zao wenyeviti wa kamati za bunge waliotajwa kuhusika na kashfa mabilioni ya fedha katika za Escrow.
Kwa upande wake kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni ni Mhe. Freeman Mbowe  amewata viongozi kutambua kuwa wanamamlaka ya kulinda rasilimali za nchi na kumtaka waziri mkuu kuwa mkali zaidi kwa kuchukua hatua na asisubiri mpaka bunge lifikie katika hatua ya mivutano,huku makamu mwenyekiti wa kamati ya PAC Mhe. Deo filikunjombe amepongeza  bunge kukubali kamati hiyo. 
Waziri wa nchi ofisi ya Rais mahusiano na utaribu Mhe.Stephen Wassira amesema jambo lolote linaloweza kuvunja umoja na kurudisha nyuma maendeleo haliwezi kuwa sera  ya CCM ambapo amepongeza makubaliano yaliyofikiwa  kati ya CCM na vyama vya upinzani.
Akihitisha mkutano wa 16 na 17, waziri mkuu mheshimiwa mizengo pinda amewahakikishia wabunge na wananchi kwa ujumla kuwa serikali itaendelea kusimamia rasilimali za nchi kwa faida ya watanzania wote, na kuahidi wale wote watakao patikana na jinai za kuvunja sheria za nchi watachukuliwa hatua.Ambapo ameahirisha bunge hadi tarehe 27 Januari mwakani.


HIZI HAPA DONDOO MUHIMU ZA KIKAO CHA LEO CHA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,MWANZO HADI KUAHIRISHWA(Kwa mujibu wa Jamii Forums)

MWANZO Kikao cha bunge kimerejea tena na wabunge ndio wanaingia bungeni huku wakimsubiri spika wa bunge aingie bungeni tayari kwa kuanza kikao. Vikao vya bunge kwa leo vimeahirishwa mara mbili. Spika wa bunge aliagiza pande zote mbili waweze kuridhiana.

Spika wa bunge na katibu wa bunge ndio wanaingia bungeni tayari kwa kuanza kikao cha bunge. Zitto amesoma maazimio mapya baada ya kuondolewa ya zamani.

Azimio: TAKUKURU na Polisi wamchukulie hatua bwana Sethi, na kumfungulia mashitaka akithibitika

Azimio: Serikali ichukue mitambo ya IPTL na iikabidhishe kwa TANESCO

Azimio: Serikali ipitie upya mikataba ya Umeme na itoe taarifa kabla ya kumalizika kwa mkutano ujao wa bunge la Bajeti

Azimio: Kwa kuwa majaji walihusika, Rais aunde Tume ya kijaji ya uchunguzi na kuwasimamisha jaji Mujulusi na Prof Luhangisa

Azimio:
 Mamlaka husika ziitangaze Benki ya Stanbic na benk yoyote nyingine itakayogundulika kuwa zinahusika na utakatishaji

Azimio: Mamlaka ya uteuzi iwawajibishe na inashauriwa kutengua uteuzi wa Prof Tibaijuka, Prof Muhongo, Jaji Werema, Maswi

Azimio: Bunge liwawajibishe wabunge ambao ni sehemu ya bodi ya TANESCO na viongozi wa Kamati za Bunge

Mbowe ametoa nasaha zake na kumuomba waziri mkuu awe mkali kuepusha mitafaruku ziku zijazo.

Filikunjombe naye anaongea, amesema wameacha uchama na kuwa wamoja katika kuwatetea watanzania na kuahidi kwa watanzania kuwa watazidi kufanya kazi vizuri na kwa uaminifu zaidi kwa niaba ya kamati pia anazungumzia kukesha kwao kulina ripoti mafisadi wasije kuipata na hatua stahiki itachukuliwa kwa kila mmoja

Wassira: Nilikua miongoni mwa wajumbe sita kuwakilisha katika kikao cha maridhiano, jana hali ilikua mbaya sana na tulitoka katika mazingira yasiyoeleweka lakini kwenye binadamu hapaharibiki jambo kumbe tukitumia busara jambo gumu linakuwa rahisi. 


Tumebadilishana mawazo kwa uaminifu zaidi, kwa niaba ya CCM tunashukuru kwa mjadala na CCM imeshiriki katika kufikia maazimio. Jambo lolote lenye kuleta msukosuko katika nchi haliwezi kuwa sera ya CCM hivyo tunaomba wananchi wayaunge mkono hayo tuliyokubaliana.

 Kama Zitto alivyosema tumegusa kila muhimili lakini tumeyagusa kwa nia njema, naunga mkono hoja.

Wabunge wameafiki japo Ole Sendeka alikuwa anataka muongozo kabla ya kura ya ndiyo.

Sendeka: Hakuna eneo linaloeleza kwamba taarifa kuwa hizi zitaletwa kwenye bunge hili tukufu, ni lazima taarifa irudi tena hapa kwenye bunge. Azimio la namna hii ni vizuri liwekewe taratibu.

Makinda: Swala hili limetikisa nchi, kamati zipo hivyo tuaminiane na nawashukuru kwa kazi nzuri mliyofanya na katibu anatoa hoja ya kuahirisha bunge.

Pinda: Leo tunahitimisha mkutano wa 16 na 17, ulijumuisha kazi kubwa zifuatazo(anazitaja) na anasema atazingatia maoni na ushauri kutoka kwa wajumbe, anaelezea maswali yaliyoulizwa pia anaongelea mgogoro wa wakulima na wafugaji wilaya ya Kiteto pia anaongelea biashara haramu ya pembe za ndovu kati ya Tanzania na China, kuchaguliwa Anna Makinda kwenye bunge la SADC.


 Anaomba kwa niaba ya serikali, atahakikisha maazimio yote yaliyopitishwa yatasimamiwa kama yalivyoazimiwa na watawasilisha bungeni matokeo ya kazi waliyoifanya. 

Yapo mapendekezo mahsusi 14 kutekelezwa na serikali, tutahakikisha yanafanyiwa kazi kikamilifu. Yaliyopita si ndwele hivyo tugange yajayo. Serikali itaendelea kusimamia mali za taifa na kulindwa, wale wote watakaopatika kwa ushahidi wa kutosha wataadhibiwa na sheria za nchi yetu.

 Naitwa bango kitita kwa sababu huwa nahakikisha kila kitu kinatekelezwa ndani ya muda. Kwa nia njema, nilisemee, Je fedha za escrow ni za umma? CAG aliacha mwanya na serikali italifanyia jambo hili kwa kina na serikali italifanyia uchunguzi kwa kina na kuja na majibu. 

Naomba niseme, jambo muhimu pia ni kuteremsha bei ya umeme kwa watumiaji wetu, tutahakikisha serikali inalipwa kwa fedha ambazo ni za umma, nilichijifunza leo kumbe mambo mengi yanawezekana kwa kupitia kamati ya maridhiano tena ndani ya muda mfupi.

Nakushukuru Spika na wabunge, serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika 14 desemba 2014 na maandalizi ya msingi yamekamilika.

HITIMISHO: Niwashuru waliofanikisha mkutano huu, niwashukuru PAC na kamati ya maridhiano(anashukuru makundi mbalimbali na safari njema wanaporudi pia sikukuu ya Chrismas na anatoa hoja kuahirisha bunge mpaka 27 January 2015 saa tatu asubuhi.

Spika anatoa nasaha zake kwa wabunge, wimbo wa Taifa unaimbwa. Anawahoji wabunge na anaahirisha bunge mpaka januari mwaka 2015 

==================

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527