MFANYABIASHARA AUAWA KINYAMA SHINYANGA,ADAIWA KUFANYIWA UMAFIA NA MFANYABIASHARA MWENZAKE

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha 
Mfanyabiashara mmoja aitwaye Mgaka Meleka(42) mkazi wa kata ya Mwakitolyo wilaya ya Shinyanga vijijini amekutwa ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kwenye ubavu wake wa kushoto na kifuani upande wa kushoto na watu wasiojulikana.

Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha tukio hilo limetokea jana saa nne asubuhi katika kitongoji cha Kitalama katika kijiji cha Mwakitolyo ambapo mwanamme huyo alikutwa ameuawa kwenye kichaka nje kidogo ya kitongoji hicho.

Chanzo cha tukio inasadikiwa kuwa marehemu alikuwa na ugomvi na mfanyabiashara mwenzake aitwaye Balu Clement (35) mkazi wa Mwakitolyo.

Kamanda Kamugisha amesema mnamo  tarehe 27,Agosti 2014 mtuhumiwa alikwenda dukani kwa marehemu na kutishia kumuua.

Mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi

Na Kadama Malunde-Shinyanga

TAFADHALI BOFYA HAPA U LIKE PAGE YETU TUKUTUMIE "HABARI" MOJA KWA MOJA KILA ZINAPOTOKEA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post