YAFAHAMU MADHARA YA COMPUTER NA SIMU ZA MKONONI


WATANZANIA wametakiwa kuwa makini wanapotumia simu na kompyuta, kwani ndio chanzo cha matatizo mbalimbali yakiwemo ya kutoona, kutosikia, upungufu wa nguvu za kiume na vifo.

Mshauri wa masuala ya teknolojia, Alex Mpompo aliyasema hayo juzi kwenye semina inayohusu teknolojia katika Parokia ya Roho Mtakatifu Segerea, Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

Mpompo alisema matatizo yanayochangiwa na teknolojia yapo mengi ikiwamo kutoona, kutosikia, upungufu wa nguvu za kiume na vifo.

Alisema vijana wengi nchini wana upungufu wa nguvu za kiume jambo linalochangiwa na matumizi mabaya ya teknolojia hivyo kuchangia familia kusambaratika.

Aliwaasa Watanzania kutotumia kompyuta kwa muda mrefu kwa kuipakata kwenye mapaja, kwani mionzi inapenya kwa urahisi katika maeneo hayo na kuathiri mbegu za kiume na kusababisha ugumba.
Watu wengi hawaelewi kama ukiweka simu karibu na jiko la gesi unaweza kuunguza nyumba, pia unapogandamiza simu na ngozi inasababisha saratani ya matiti na ugonjwa wa moyo
alisema Mpompo.

Alisema vijana wanaoongea na simu kwa muda mrefu wapo kwenye hatari zaidi ya kupoteza kumbukumbu na kutosikia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527