WACHEZAJI HAWA WAWILI HAWATOICHEZEA MANCHESTER UNITED KESHO

United_2869643b
Klabu ya Manchester United leo mchana imesafiri kuelekea jijini Munich kwa ajili ya kupambana na Bayern Munich katika mchezo wa pili wa hatua ya 16 bora.Katika listi ya wachezaji waliosafiri na timu hiyo jina la mshambuliaji Wayne Rooney lilikuwepo pamoja kwamba iliripotiwa anaweza asiichezee timu hiyo kesho, lakini majina ya kiungo Marouane Fellaini na mlinzi Rafael hayakuwemo katika listi ya wachezaji waliosafiri na timu kwenda Munich ikielezwa kwamba wana majeruhi na hivyo hawataichezea timu hiyo.

United tayari imewasili Ujerumani na leo jioni walifanya mazoezi katika uwanja wa Allianz Arena kujiandaa na kipute cha kesho.
Timu hizo zilitoka sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza uliopigwa Old Trafford wiki iliyopita.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post