HABARI PICHA-NAPE NA KINANA WATUA KIGOMA KWA AJILI YA ZIARA YA SIKU 5

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dk. Walid Kaborou akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma. Pichani nyuma ni Mjumbe wa NEC,Balozi Ali Karume walipowasili jioni ya leo kwa ziara ya siku tano mkoani Kigoma.
 Viongozi mbalimbali wa ngazi za juu za chama cha CCM Taifa na Mkoa wakiwa uwanja wa ndege mapema leo jioni ,mjini Kigoma wakimsubiri kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisindikizwa na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa Dk. Kaborou wakati akipita katika paredi la UVCCM alipopokelewa Uwanja wa Ndege wa Kigoma jioni ya leo.

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisalimiana na Katibu wa NEC Siasa,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye,Mkuu wa mkoa wa Kigoma,Kanali Mstaafu Issa Machibya na Kamanda wa Vijana na Mchumi wa CCM mkoa wa Kigoma,Ndugu AbdulKadir Mushi mara alipowasili jioni ya leo kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Kigoma,Kanali Mstaafu Issa Machibya jioni ya leo mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma.

Sehemi ya Waendesha boda boda wakiupokea msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mapema leo jioni,mara baada ya kuwasili mjini Kigoma.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post