Vituko vya Dunia!! WANAUME VIFUA WAZI WAPIGWA MARUFUKU NCHINI UINGEREZA

Wanamme wakiwa vifua wazi eneo la bustani ya Adventure Island.

Wanaume wanaovua mashati wamepigwa marufuku kuitembelea bustani ya mapumziko na kujivinjari ya Adventure Island.
Ni eneo ambalo watu wanakwenda kujivinjari na familia zao, kwa kutazama wanyama, watoto hupata kubembea na pia watu huota jua.

Mkurugenzi mkuu, Marc Miller, amesema anataka wanaume waonyeshe "ustaarabu".Bustani hiyo iliyopo mjini Southend nchini Uingereza, imeweka ilani zinazowaomba wanaume wasivue mashati yao, na kwamba watakao patikana watafukuzwa.


Adventure Island inasema imeidhinisha marufuku hiyo kuzivutia familia.

Bustani hiyo inasifika duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya watu walio uchi walioipanda bembea ya 'Rollercoaster' - licha ya kwamba ni jambo linalofanyika faraghani.
'Kuilenga Familia'

Zaidi ya watu 100 walivua nguo ili kuipanda bembea hiyo ijulikanayo kama Green Scream mnamo 2010.

Miller anasema: "Katika miaka ya hivi karibuni, tumekuwa tukiongeza idadi ya vijana na wanaume ambao huvua mashati yao ili kupata joto la jua kwa wingi. Hilo ni sawa kabisa lakini katika mazingira yanayofaa".

"Tunajaribu sana kufanya biashara inayoivutia familia na sio kila mtu anavutiwa kuona vifua wazi".

Pamoja na kuwa na idadi kubwa duniani ya watu w
asio vaa nguo, Adventure Island pia ilijaribu kuweka rekodi mpya ya kuwa na watu wengi wanaocheza mpira wa gofu wakiwa uchi, mnamo mwaka 2012.

Msemaji mmoja anasema michezo yote hufanyika faraghani.
"Wanaohudhuria michezo hiyo ni waliojisajili kushiriki, ili kuchanga fedha nyingi za misaada ya kukabiliana na magonjwa kama saratani ya matiti na ya uume," alisema.


"Marufuku hiyo imetolewa wakati bustani imefunguliwa kwa umma."
via>> BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post