VIJANA WASIO NA KAZI WAPEWA ELIMU YA USHAURI MANISPAA YA SHINYANGA

 
Vijana waliomaliza elimu ya sekondari na kushindwa kuendelea na masomo ya elimu ya ngazi ya juu katika manispaa ya shinyanga wameshauriwa kujiunga na vyuo  mbalimbali hapa nchini ili kujenga taifa la watu wasomi badala ya kukaa vijiweni

Hayo yamezungumzwa jana na mratibu wa kongamano la Elimu ya Ushauri Walter Lema kutoka chuo cha usimamizi wa Fedha cha Luther kilichpo jijini Mwanza, wakati akitoa elimu ya ushauri kwa vijana waliomaliza elimu ya kidato cha Nne na kuendelea  mjini Shinyanga ambao hawana taaluma yeyote na kuamua kukaa nyumbani bila kazi.


Elimu hiyo imetolewa katika viwanja vya Mazingira senta Mjini Shinyanga  kwa lengo la kuwasaidia vijana waliokata tamaa na maisha kubadilika na kuzitumia fursa zinazopatika na hapa nchini.
 
Alisema vijana wengi hapa nchini wamekuwa wakikata tamaa na maisha  pale wanaposhindwa kujiunga na elimu ya juu na kuamua kukaa nyumbani bila kazi hali ambayo inachangia kuongezeka kwa idadi kubwa ya vijana kutokuwa na ajira

Naye mwezeshaji wa pili wa elimu hiyo bi Upendo Dickson aliwataka vijana hao pale wanapotaka kujiunga na vyuo hivyo vya Taaluma wachague fani ambazo zitawapatia fursa ya kupata ajira kwa urahisi ikiwani pamoja na kuchagua fani ambayo wanaipenda na sio kushinikizwa

Bi Dickson alisema  hivi sasa hapa nchi kuna fursa nyingi ambazo zinapatikana tofauti na kipindi cha nyuma, hivyo vijana na wanatakiwa kuzitumia fursa hizo kwa kujipatia kipato na kuinua uchumi wa Taifa kuliko kukaa nyumbani bila kazi huku akisema kuwa kufeli mtihani sio kufeli maisha

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post