Ukatili wa aina yake!!! BABA ATESA MTOTO WAKE ILI AFE KISA HAPENDI WATOTO WA KIUME,AMVUNJA VIDOLE,AMBANIA CHAKULA,ATISHIA KUUA MKE WAKE KAMA ATASEMA


Mtoto Amos Baya mwenye umri wa miaka minne ambaye toka kuzaliwa kwake amekuwa akipata mateso kutoka kwa baba yake kisa kwanini kazaliwa wa kiume,hali iliyosababisha mtoto huyo kudhoofika mwili na kupata ugonjwa wa utapiamlo

Vidole vya mtoto Amos Baya kama vinavyoonekana hapo vimevunjwa haviwezi kunyooka

Wakati watu wengine wanakesha kila siku kutafuta watoto lakini pia wadau mbalimbali wakiendelea kupiga vita ukatili dhidi ya wanawake na watoto,lakini vitendo hivyo vimeendelea kujitokeza katika jamii ambapo huko katika kijiji cha Senane wilayani Maswa mkoa mpya wa Simiyu mwanamme mmjoa aitwaye Baya  Seni amekuwa akimpa mateso makali mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka minne ili afe kwa madai kuwa hapendi watoto wa kiume.

Baya Seni ambaye ni mkazi wa kijiji hicho cha Senane amekuwa akimpa mateso makali mtoto huyo anayejulikana kwa jina la Amos Baya mwenye umri wa miaka minne toka kuzaliwa kwake hali  iliyoelezwa kusababisha mtoto huyo kudhoofika mwili na kupata ugonjwa wa utapiamlo.

Miongoni mwa mateso aliyoyapata mtoto huyo ni pamoja na kuvunjwa vidole vya mkono wa kushoto, kutelekezwa shambani siku zaidi ya mbili bila kula na kuning'inizwa juu ya mti.

Imeelezwa kuwa Mwanamme huyo hapendi watoto wa kiume kwa madai kuwa wanaleta umaskini kwa sababu wakikua watataka kuoa na kuchukua mali, lakini mtoto wa kike akikua ataolewa na kuleta mali nyumbani.

Taarifa za mtoto huyo kupata mateso kutoka kwa baba yake mzazi zilitolewa na msamaria mwema   siku ya tarehe 31 mwezi Machi mwaka huu  ambaye alikwenda katika shughuli za mazishi katika kijiji hicho na kumwona mtoto huyo ndipo akapiga simu ofisi ya ustawi wa jamii wilaya ya Maswa na kufuatia taarifa hizo ofisi hiyo iliwataarifu polisi na wakaenda kumchukua mtoto huyo na kumuweka chini ya ulinzi baba mzazi wa mtoto huyo.

Afisa ustawi wa jamii wilayani maswa Bwana Husein Mshana amethibitisha kutokea kwa tukio hilo

Hivi sasa mtoto huyo amelazwa wodi namba nane ya watoto katika hospitali ya wilaya ya Maswa akipatiwa matibabu.
Mama mzazi wa mtoto huyo  Elizabeth Paul amekiri kuwa mtoto huyo amekuwa akifanyiwa vitendo vya ukatili na baba yake mzazi na kwamba hata yeye  amekuwa akipewa vitisho kuwa endapo atasema atauawa.

Tayari baba mzazi wa mtoto huyo Amos Baya anashikiliwa na jeshi la polisi wilayani maswa kwa hatua za kisheria.
Na Veronica Natalis-Simiyu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post