Ukistaajabu ya Musa........!!!! JAMAA AJARIBU KUJIZIKA KUKWEPA MATATIZO YA NDOA


Mwanamume mmoja nchini Kenya aliwaacha wakazi wa
kijiji cha Tivani mkoa wa Bonde la uffa vinywa wazi baada ya kujichimbia
kaburi na hata kujaribu kujizika mwenyewe kutokana na alichosema ni
matatizo ya ndoa.

Kwa mujibu wa kituo cha runinga cha KTN nchini
Kenya, tukio hilo lililotokea Jumanne asubuhi na kuwashangaza wakazi wa
eneo la Trans Nzoia mkoa wa Rift Valley


Mwanamume huyo, alidai kuwa ana matatizo ya ndoa
ambayo yeye mwenyewe ameshidwa kuyatatua na kwa hivyo kwake
kilichosalia ni kwenda mbinguni.


Alisema mkewe alikuwa amemwambia jambo ambalo lilimkera roho na ndhio maana akaamua kujitoa uhai.


Mwanamume huyo kwa jina Kipsang , alichimba
kaburi hilo usiku na hata kujaribu kujizika akiwa hai wakati mkewe na
watoto wake walipokuwa wanalala.


Wanakijiji katika kijiji cha Tivani walikuwa na
wasiwasi kuwa mwanamume huyo alikuwa amerukwa na akili ingawa walikiri
kwamba yeye na mkewe wamekuwa wakikumwba na matatizo ya ndoa.


Mkewe alisema kuwa amechoshwa na mwanamume huyo ambaye ametelekeza familia na majukumu yake.


Baba huyo wa watoto wawili ambaye ni kondakta wa
matatu, hatimaye aliondoka katika kaburi hilo baada ya wanakijiji
kumsihi huku wazee wakiwataka watu kupanda migomba ya Ndizi neneo
alilokuwa amechimba kaburi hilo ili kuzuia mikosi.chanzo BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post