MWANAMUZIKI MKONGWE NCHINI TANZANIA MUHIDIN MAALIM GURUMO AFARIKI DUNIA

 
Mwimbaji Mkongwe wa Bendi ya Msondo Ngoma, Muhidin Maalim Gurumo amefariki  dunia mchana wa leo.Ni mzee wa siku nyingi sana kwenye muziki Tanzania,amekuwa kwenye bendi hiyo zaidi ya miaka 50,ni mzee ambae aliwahi kuingia kwenye vichwa vya habari mara nyingi hasa kutokana na kuugua kwake kuliko mfanya aache hata muziki aliokua anaufanya.

Taarifa zilizothibitishwa na hospitali ya Taifa Muhimbili  zimesema Mzee huyu amefariki dunia akiwa hospitalini hapo leo April 13 2014 saa nane mchana baada ya kuletwa jana asubuhi na kulazwa kwenye wodi namba 6 ya Mwaisela kutokana na kuzidiwa.
Imeelezwa kuwa mzee Gurumo amefariki kutokana na maradhi ya moyo.

Tayari mwili wake umepelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti na kwamba msiba uko nyumbani kwake Mabibo Makuburi.Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya marehemu Gurumo.Amina!!

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post