Ni balaa!!! MPESYA CUP YAANZA KUTIMUA VUMBI HUKO KAHAMA,TAZAMA PICHA HAPA


 Maandamano ya kuelekea katika uwanja wa Taifa Mjini Kahama yaliojumuisha Timu 26 tayari kwa ufunguzi wa mashindano ya Mpesya Cup
 Mkuu wa Wilaya ya Kahama  Benson Mpesya akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Ngaya FC katika uzinduzi wa mashindano ya Mpesya CUP yalionza juzi Wilayani Kahama
 Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya akifungua mashindano ya Mpesya Cup yatakayosaidia kupata Timu ya Wilaya ya Kahama
 Baadhi ya Timu zilizoshiriki katika maandamano ya ufunguzi wa mashindano ya Mpesya CUP
 Wachezaji wa Timu mbalimbali wakiwa katika maandamno
Wa kwanza kulia Mwenyekiti CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja ambaye pia alikuwa mmoja kati ya Viongozi walioshiriki katika maandamano hayo,wa kwanza kulia ni bwana Raymond Mihayo wa gazeti la Habari leo na mihayorj.blogspot.com
  Wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya Kahama Benson Mpesya na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja(wa kwanza kutoka kulia) wakiwa katika maandamano.
 
Serikali Wilayani Kahama Mkoa wa  Shinyanga imesema kuwa haitawatupa Vijana hasa katika masuala mazima ya michezo kwa lengo la kuinua uchumi wa Wilayani hiyo sambamba na kupata timu itakayoshiriki ligi kuu kwa miaka ijayo.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama  Benson Mpesya aliyasema hayo wakati akifungua mashindano ya Mpira wa miguu maarufu kama Mpesya cup ambayo yanashirikisha jumla ya timu 26 za Wilaya ya Kahama.

Mpesya alisema kuwa haiwezekani Wilaya ya Kahama pamoja na kuwa rasilimali nyingi ikiwemo wawekezaji katika sekta za migodi na Tumbaku wapo lakini Wilaya  inakosa timu inayoshiriki ligi kuu hapa nchini.

Alisema lengo la mashindano ya Mpesya cup ni kukuza vipaji kwa Vijana wa Wilaya ya Kahama sambamba na kutafuta wachezaji ambao wataunda timu ya kombaini ya Wilaya ya Kahama ambayo itashiriki katika mashindano mbalimbali.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Kahama alisema mpira ni starehe  na unakuza akili  na kuongeza kuwa hivi  sasa pia ni ajira hali ambayo itawafanya wachezaji kufanya michezo kama sehemu yao ya kujipatia kipato.

“ Kwa sasa tumedhamiria ,Wilaya ya Kahama lazima tupate timu itakayocheza ligi kuu ,Rasilimali tunazo,wachezaji tumieni michezo katika kuonyesha vipaji vyenu ”, Alisema  Mpesya.

Pia aliwataka wachezaji kutumia michezo kama sehemu ya kujenga urafiki  na mahusiano mazuri na kutoa onyo kwa waamuzi mashindano hayo kuhakikisha kuwa wanachezesha michezo hiyo kwa kufuata sheria 17 za soka.

Katika michezo hiyo hiyo ya Mpesya cup mshindi wa kwanza atapata zawadi ya shilingi milioni moja pamoja na seti moja ya jezi, kikombe  na mpira mmoja wakati wa pili atapa kiasi cha shilingi 500,000 pamoja na seti moja ya jezi na mpira .

Michuano hiyo tayari imeanza juzi kwa mechi moja katika timu ya Ngaya FC na Ambassador na kumalizika kwa matokeo ya timu ya Ambassador kuinfunga timu ya Ngaya FC kwa jumla ya mabao 2-1.
picha na stori kwa hisani ya  mihayorj blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post