Ni balaaa!!! PSPF WAKUTANA NA WAFANYABIASHARA MJINI SHINYANGA, WATOA ELIMU KUHUSU MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI,FUATILIA HAPA TUKIO ZIMA

Ni katika siku ya kwanza ya ziara ya afisa kutoka mfuko
wa pensheni wa PSPF (Public Service Pension Fund),Erick Chanimbaga,akiwa ameambatana na mjumbe wa bodi ya PSPF bwana  Clement Mswanyama,mkoani Shinyanga iliyoanza leo inayolenga kutembelea na kuhamasisha  wafanyakazi katika sekta binafsi wakiwemo wafanyabiashara,wafanyakazi wa viwandani,waendesha bodaboda na wajasiriamali wa aina mbalimbali kwa ajili ya kuwafahamisha,kuwahamasisha na kuwaelisha kuhusu mpango wa uchangiaji wa hiari(pspf supplimentary scheme),mpango ambao umeanzishwa na PSPF kwa ajili ya kupanua wigo wa uanachama kwa kuandikisha wananchi waliojiajiri au kuajiriwa katika sekta rasmi na isiyo rasmi.Kulia ni Clement Mswanyama mjumbe wa bodi ya PSPF akizungumzia lengo la ziara yao,kushoto kwake ni afisa mfawidhi PSPF mkoa wa Shinyanga Erick Chanimbaga wakizungumza na wafanyabiashara katika soko kuu la mjini Shinyanga jioni ya leo
Kulia ni Afisa mfawidhi PSPF mkoa wa Shinyanga Erick Chanimbaga akieleza kuhusu namna ya wanachama wa mpango wa uchangiaji hiari watakavyoweza kuwasilisha michango yao,ambapo alisema kuna namna tatu za kuchangia kama vile kwa wiki,mwezi au msimu kutegemea na upatikanaji wa kipato cha ziada kwa ajili ya akiba.Alisema michango hiyo itawasilishwa moja kwa moja kupitia akaunti ya benki au kwa wakala wa malipo wa M-PESA,TIGO PESA NA AIRTEL MONEY,ambapo kiwango cha uchangiaji ni kuanzia shilingi elfu kumi au zaidi.Alisema ofisi za PSPF katika mkoa wa Shinyanga zipo kwenye jengo la Benki ya posta ghorofa ya pili.

Aidha  Chanimbaga aliwaambia wafanyabiashara hao kuwa  mara baada kujiunga na mfuko huo wanawezpa kupata taarifa zao njia tatu ambazo ni kwa kupiga simu  namba 0225510400 ambayo ni kwa ajili ya huduma kwa wateja kwa njia ya simu, pia kwa kutumia huduma nyingine iitwayo pspf karibu nawe kwa kutuma ujumbe wa mfupi wa simu andika neno pspf kwenda namba 15357 au kwa kutembelea ofisi zozote za pspf,na kwa njia hizo anaweza kupata historia ya michango yake tangu mwanzo 

Kushoto ni mwenyekiti wa soko kuu mjini Shinyanga bwana Alex Stephen,kulia kwake ni afisa masoko wa manispaa ya Shinyanga bwana Mabina Amani wakiwa ndani ya soko kuu wakifuatilia kilichokuwa kinazungumzwa na afisa pamoja na mjumbe wa bodi ya PSPF ambao walisema mfuko wa hifadhi ya jamii umepanuliwa ili watu kutoka katika sekta binafsi ili wanufaike na mfuko huo
Kulia ni mfanyabiashara katika soko kuu la mjini Shinyanga bwana Apolinari Mabula akifuatilia kwa umakini zaidi swali alilouliza kwa afisa kutoka PSPF mkoa wa Shinyanga na mjumbe wa bodi ya PSPF  kuhusu namna ya kuchangia na endapo kuna mafao yoyote kupitia mpango huo wa uchangiaji hiari

Kushoto ni bwana Clement Mswanyama mjumbe wa bodi ya PSPF akitaja aina ya mafao yaliyopo katika mpango wa uchangiaji  wa hiari,ambapo alisema kuna mafao ya aina sita kama vile fao la Elimu,fao la ujasiriamali,fao la uzeeni,fao la kifo,fao la ugonjwa pamoja na fao la kujitoa.Mswanyama alisema ni wakati mzuri sasa kwa vijana kutumia fursa hiyo ya uchangiaji wa hiari kuweka akiba ya uzeeni ili wasipate taabu wakiwa wazee kwani fao hilo litalipwa kwa mwanachama aliyefikisha umri wa miaka 55 au zaidi ambapo mwanachama atalipwa akiba yake ya asilimia mia moja pamoja riba itakayokokotolewa.


Kulia ni bwana Clement Mswanyama mjumbe wa bodi ya PSPF kushoto kwake ni afisa mfawidhi PSPF mkoa wa Shinyanga Erick Chanimbaga wakinong'ona jambo ndani ya soko kuu la mjinin Shinyanga wakiwa katika ziara yao kuhamasisha wafanya kazi wa sekta binafsi kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari ulioanzishwa na PSPF kwa ajili ya kupanua wigo wa uanachama kwa kuandikisha wanachama wanaojiajiri au kuajiriwa katika sekta rasmi na isiyo rasmi

Mbele ni Clement Mswanyama mjumbe wa bodi ya PSPF akizungumzia kuhusu fao la ujasiriamali ambapo alisema litatolewa kwa mwanachama ambaye amechangia kwenye mfuko kwa kipindi kisichopungua miezi 12 ambapo nusu ya akiba ya mwanachama(50% ya michango) itatumika kulipa fao hilo na nusu itabaki katika akaunti ya mwanachama kwa ajili ya akiba ya uzeeni,na katika hili mwanachama atapaswa kuandika barua ya maombi

Mbele ni Afisa mfawidhi PSPF mkoa wa Shinyanga Erick Chanimbaga,akizungumza na wafanyabiashara katika soko hilo ambapo alisema mpango wa uchangiaji wa hiari una umuhimu mkubwa kwa wafanyakazi kutoka sekta binafsi kwani uchangiaji wake unategemea na upatikanaji wa kipato cha ziada kwa ajili akiba na hakuna gharama ya kujiunga na mpango huo ila unatakiwa na picha moja ya pasipoti na hakuna ukomo wa uchangiaji
 Afisa mfawidhi PSPF mkoa wa Shinyanga akiwa ameambatana na mjumbe wa bodi ya PSPF kesho siku ya Ijumaa wataendelea na ziara yao mkoani Shinyanga ambapo wanatarajia kukutana na waendesha bodaboda,wafanyakazi wa viwandani na wajasiriamali pamoja na makundi ya aina mbalimbali mjini Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post