Breaking News!!! KANISA KATOLIKI LAPATA MSIBA-PAROKO WA GEITA MJINI AFARIKI DUNIA


Vilio vimetawala miongoni mwa  waumini wa kanisa katoliki jimbo la Geita katika kanisa la Bikira Maria wa Fatma la mjini Geita kufuatia taarifa  za kifo cha poroko wa parokia ya Geita Padri Henry Kimisha aliyefariki ghafla leo asubuhi katika hospitali ya wilaya ya Geita baada ya kuugua ghafla.

Akitoa taarifa za kifo hicho hilo leo msaidizi wa askofu jimbo la Geita Pdr Nikodema Duba amesema  paroko huyo amefariki dunia saa 2 asubuhi baada ya kuugua ghafla na kulazimika kumpeleka hospitali ya wilaya ya Geita na wakati wakifanya maandalizi ya kumpeleka hospital ya mission Sengerema ghafla akakata roho.

Aidha msaidizi wa askofu huyo amesema  paroko huyo alikuwa anasumbuliwa na shinikizo la damu(presha) hivyo na muda huo hali yake ilibadilika ghafla kiasi cha kumpeleka hospitali haraka lakini mwenyezi mungu akamchukua.

Baadhi ya waumini na wasio waumini wa kanisa katoliki wameshtushwa na kifo cha paroko huyo ambaye wanamfahamu na amekuwa akishirikiana nao katika mambo ya kijamii na shughuli mbalimbali zilizokuwa zinahusu jamii hiyo.

Naye katibu wa parokia hiyo Bw,Mansety Kyara amemlilia paroko huyo na kuongeza kuwa walikuwa katika maandalizi ya kumuaga Baba askofu Damian Dallu aliyehamishiwa jimbo la Songea mkoani Ruvuma.

Padri kimisha alizaliwa tarehe 8/6/1967 katika kijiji cha katunguru wilayani Sengerema mkoani Mwanza na alipata daraja takatifu ya  upadri tarehe 25/7/1996 katika parokia ya nyantakubwa wilayani sengerema na mazishi yake yatafanyika ijumaa katika makaburi ya kanisa hilo ambapo mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa Bugando.

 Mungu ailaze mahali pema mbinguni roho ya marehemu Henry Kishima,Amina!!!
 Na Valence Robert Geita


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post