BASATA YATUMA SALAM ZA RAMBI RAMBI KIFO CHA MWANAMUZIKI MKONGWE MZEE GURUMO ALIYEFARIKI JANA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh2lVMZBoySATQ2CiybPMhTqR7N8HJb9Ag7UeZKeJgKJy1ZbqyKrPNocnAF3Ae0CJmHBzegwDptI7wpA_myAv9vilj86dw3XMLFRVLnD_bP8Lk3AJJE5lIXA6HlCbuIdJSbY9C1Zs2ow1Ag/s1600/New+Picture+(3).png
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa msanii nguli wa tasnia ya muziki wa Dansi nchini Muhidini Maalimu Ngurumo 
 

“ Baraza limestushwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa ya kifo hiki cha Muhidini Maalimu Ngurumo ambaye mchango wake katika muziki wa dansi ni mkubwa mno na  unahitajika sana, pengo aliloliacha ni kubwa kwani ubunifu wake bado unahitajika katika tasnia hii.”


 Baraza linatoa pole kwa familia ya marehemu na wasanii wote nchini, aidha tunawatakia moyo wa subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na mpendwa wetu.
 

Mwenyezi Mungu aipumzishe mahala pema peponi roho ya marehemu. Baraza liko pamoja na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.Imetolewa na

Godfrey Mngereza

Kaimu Katibu Mtendaji

Baraza la Sanaa la taifa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post