TRAFIKI AMSHUSHIA KIPIGO MWENDESHA BODABODA,ALIKUWA AMEPAKIZA ABIRIA ZAIDI YA MMOJA-"MSHIKAKI'

  Jamaa akionesha uso wa huzuni baada ya kichapo kutoka kwa trafiki
 
Askari wa usalama barabarani (hayupo pichani) anadaiwa kumjeruhi dereva bodaboda eneo la vingunguti jijini Dar es salaam. 
Chanzo chetu cha habari kimeeleza kuwa, tukio hilo limetokea jana majira ya mchana wakati dereva huyo alipokutana na askari akiwa amebeba abiria wawili maarufu kama"mshikaki". 
 
Imeelezwa kuwa baada ya askri huyo kutaka kupata maelezo ya kina kutoka kwa dereva huyo, ndipo ikatokea hali ya kutoelewana kati yao ndipo askari huyo aliamua kumzaba kibao na kumjeruhi kama picha unavyoona picha ya jamaa hapo juu.
Na Haruni Sanchawa-Dar 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post