Noma sanaaa !!! HIRIZI YATUMIKA KUIBA MTOTO HUKO GEITA,WANANCHI WAMSHUSHIA KIPIGO CHA MAANA MWANAMKE MWIZI WA MTOTO


 
Mtoto mmoja aliyejulikana kwa jina la Vick Pita (3) amenusurika kuibiwa na mwanamke mmoja aliyedaiwa kutumia hirizi kumfanyia manyanga mtoto huyo katika mtaa wa Bomani kata ya kalangalala wilayani Geita mkoani Geita.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana katika kata kata ya Kalangalala wilayani humo.

Akisimulia juu ya tukio hilo mama mdogo wa mtoto huyo Frola Samson  amesema tukio hilo limetokea wakati akimsafirisha kwa pikipiki mtoto huyo pamoja na mwingine aitwaye Happiness Peter (2) kuwapeleka
 kwa baba yao anayefanya kazi umbali wa kilomita 1 kutoka nyumbani kwao.

Amesema mara baada ya kuwapakia watoto hao kwenye pikipki maarufu kama bodaboda mama mmoja akiwa na hirizi  ambaye hakujitambilisha jina lake alikuja na kuanza kumkumbatia mtoto huyo na kudai kuwa ni mtoto wake na kumbatiza jina la bandia la Glory.

Ameongeza kuwa baada ya kumbatiza jina hilo bandia mama huyo alimwamuru mwenye bodaboda kuondoka kwa kasi lakini mwendesha bodaboda  huyo alipoona mtoto analia aliondoka eneo hilo peke yake na kumwacha mama  huyo aliyefahamika kwa jina la Neema Mazura(18) akiendelea kumkumbatia mtoto Vick .

Ameongeza  kusema kuwa mwizi huyo aliyekuwa na hirizi kichwani na mkononi alikuwa akimfanyia manyanga mtoto huyo kwa kumzungushia hirizi mkononi.

Kufuatia hali hiyo mama mdogo wa mtoto huyo Flora Samson  alirudi  nyumbani kumfuata mama  mzazi wa mtoto huyo na kumpa habari kuwa mwanaye anaibiwa na muda mfupi watu walikusanyika na kuanza kumshushia kipigo mama huyo kwa kitendo hicho cha kutaka kuiba mtoto.

Kitendo cha kutaka kuibiwa kwa mtoto huyo kimewaweka macho wazi wakazi wa mtaa huo na kusikika wakisema auawe  kwani wamezidi kuwaiba  kwa kutumia madawa yao na kwenda kuwatoa kafara watoto hao.

Jeshi la polisi mkoani Geita linamshikilia mtuhumiwa huyo na atafikishwa mahakani baada ya upelelezi kukamilika.

Na valence Robert -Geita.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post