JAMAA AUAWA KWA KUTAFUNWA NA FISI AKITOKA KUNYWA POMBE HARAMU (GONGO) HUKO SIMIYU

 

Katika hali ya kusikitisha huku wengine wakidai kuwa ulevi ni noumaaa!!,mwanamme mmoja aitwaye Mayunga Gamaya (57)  amefariki dunia baada ya kuvamiwa ,kushambuliwa kisha kutafunwa na fisi wakati akitoka kunywa pombe haramu  aina ya  gongo katika kijiji cha Ng’hami kata Nyalikungu wilaya ya Maswa mkoani Simiyu.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Simiyu Charles Mkumbo amesema tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 10 jioni wakati mkulima huyo akitoka kunywa pombe katika moja  ya nyumba ya mwanakijiji mwenzao katika kijiji hicho akirejea nyumbani kwake na kwamba inasadikiwa Gamaya alikuwa amekunywa pombe haramu aina ya gongo na wakati akirejea nyumbani alivamiwa na fisi kisha fisi huyo kumburuza hadi vichakani na kuanza kumtafuna.

kamanda Mkumbo amesema  mwili wa merehemu ulionekana wakati wachungaji wa mifugo wakati wanarejesha mifugo yao walikokuwa wanachunga  majira ya jioni na kuona mabaki ya kichwa cha Gamaya na nguo zake alizokuwa amevaa siku hiyo zikiwa eneo la vichakani na baada ya wananchi kutambua mwili wa marehemu na jeshi la polisi kuruhusu wazike mabaki ya marehemu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post