NDOVU MNYAMA WA AJABU,ANA KUMBUKUMBU YA KUTOFAUTISHA SAUTI YA BINADAMU MWANAMME NA MWANAMKE

Katika utafiti huo ambao ulifanyika katika mbuga ya wanyama ya Amboseli nchini Kenya, imegundulika kuwa ndovu wana uwezo mkubwa pia wa kutambua sauti za watu wa makabila mbalimbali.
Ndovu wamejifunza kutambua sauti za watu kutokana na kuwepo mzozo wa maji kati ya binadamu wanaoishi karibu na mbuga hiyo na wanyama hao. Hivyo ndovu wameweza kugundua sauti za binadamu wa makabila ambayo ni adui na tishio kwao na wale ambao sio adui kwao.
Maasai wa eneo la Amboseli wanaelezwa kuwa huwa na tabia ya ukali na huwaua ndovu hao tofauti na Wakamba ambao wanakisiwa kuwa watulivu.
Zoezi lilifanyika hivi, wakati ndovu hao wanaposikia sauti ya Maasai walirudi nyuma na kujikusanaya kama wamesikia ishara ya hatari laikini waliposikia sauti za Wakamba walibaki mahala pale pale kwa utulivu.
Hivyo matokeo ya utafiti huo yameonesha kuwa ndovu wameongeza uwezo mkubwa wa kurudisha kumbukumbu ili kutambua tofatuti kati ya sauti kadhaa za makabila mbali mbali duniani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post