CRISTIANO RONALDO NDIYO MCHEZAJI WA MPIRA WA MIGUU MWENYE UTAJIRI ZAIDI DUNIANI

Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo jana (March 10) alitajwa kuwa ndiye mchezaji wa mpira wa miguu mwenye utajiri mkubwa zaidi duniani huku akimpiga kikumbo mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi.
Kwa mujibu wa orodha iliyotolewa na Goal.com, Ronaldo ana utajiri wenye thamani ya £122 Million na anafuatiwa na Messi mwenye utajiri wa £120.5 Million.
Ronaldo anachukua taji la David Beckham alilolivaa mwaka jana ambapo alipotajwa kuwa mcheza mpira tajiri zaidi kwa mwaka 2013.
Hii ni orodha ya wachezaji kumi matajiri zaidi duniani kwa mwaka 2014.
1. Cristiano Ronaldo, Real Madrid €148m (£122m)
2. Lionel Messi, Barcelona €146m (£120.5m)
3. Samuel Eto’o, Chelsea €85m (£70m)
4. Wayne Rooney, Manchester United €84m (£69m)
5. Kaka, AC Milan €82m (£67.5m)
6. Neymar & family, Barcelona €80m (£66m)
7. Ronaldinho, Atletico Mineiro €78m (£64m)
8. Zlatan Ibrahimovic, Paris St-Germain €69m (£57m)
9. Gianluigi Buffon, Juventus €63m (£52m)
10. Thierry Henry, New York Red Bulls €57m (£47m)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post