Makubwa haya!!! MFUNGWA AMWOMBA JAJI AMRUDISHE JELA MIEZI 6 ILI AMALIZIE KOZI YAKE

Akamuomba Jaji amrudishe jela miezi sita ili akamalizie kozi yake, adai itamsaidia kwa maisha ya baadae

Katika hali isiyo ya kawaida, mfungwa mmoja aliyetambulika kwa jina la Troy Smith amemuomba Jaji wa mahakama ya Canterbury, Uingereza amuongeze kifungo cha miezi sita jela ili aweze kumalizia kozi alizokuwa akizipitia wakati akiwa jela.

Mwanaume huyo mwenye miaka 41, August mwaka jana alifikishwa mahakamani hapo kwa kosa la kuvamia na kumpiga vibaya mtu mmoja na kumsababishia maumivu na kutoka damu kwenye ubongo.
Hata hivyo mtu huyo alionesha jeuri ya aina yake baada ya kukamatwa na kutupwa katika selo za polisi. Jamaa alijisaidia haja ndogo kwenye kwenye selo za polisi na inaripotiwa kuwa alimtemea mate afisa wa polisi.
Baada ya kufikishwa mahakamani alikubali makosa yote na kufungwa jela kwa kipindi cha miezi sita. Lakini baada ya kutoka, Smith akishirikiana na wakili wake walimuomba Jaji amuongeze kifungo/amrudishe jela ili akamalizie kozi yake ambayo alidai ingemsaidia sana kwa maisha yake ya baadae.
“Ningependa unipe miezi mingine sita jela kwa sababu nitaweza kumalizia kozi nilizokuwa nazipitia ambazo zitanisaidia kuelekea katika maisha yangu ya baadae.” Alisema Smith.
Kwa mujibu wa gazeti ya Kent, Jaji alikubalina na ombi hilo na kumrudisha jela kwa kipindi cha miezi sita mingine.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post