MHAMIAJI HARAMU AKAMATWA NDANI YA SANDUKU LA NGUO

 
Je, ni kwa kiasi gani uko tayari kuhatarisha maisha yako ili uweze kufikia malengo yako? Kijana mmoja kutoka Mali huko Afrika ya Magharibi akiwa na ndoto za kufika Ulaya, mahali alipokuwa na matumaini kuwa ataweza kuishi maisha yaliyo bora zaidi, baada ya kujaribu kila mbinu za kufika Ulaya na kutokufanikiwa aliamua kuvushwa akiwa amefichwa ndani ya sanduku la nguo.
 
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 19 alikubaliana na mtu mmoja kutoka Morocco ambaye alimwingiza ndani ya sanduku lake la nguo ili amvushe kutoka Morocco hadi Melilla huko Spain.
 
Lakini kwa bahati mbaya maafisa wa uhamiaji walitilia shaka sanduku hilo na kumwomba mwenyewe alifungue ili waweze kulikagua.
 
Kuona hivyo, yule kijana mwenye sanduku aliona mambo yameshaharibika. Ghafla alitimua mbio akiliacha nyuma sanduku lake. Maafisa hao walilifungua sanduku hilo na kumkuta mhamiaji huyo akiwa kajikunyata ndani.
 
Makubwa hayo ya wahamiaji haramu na ndoto za kufika Ulaya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post