NB-Picha haiendani na tukio katika habari hapa chini |
Mfungwa wa gereza la Butundwe
wilayani Geita mkoani Geita mwenye namba 224/2013 Godfrey Selemani(19)
amembaka mwanafunzi wa shule ya msingi Luhuha kata ya Nyakagomba na tarafa ya
Butundwe baada ya kumkuta anachanja kuni porini.
Tukio hilo limetokea tarehe 26/2/2014 majira ya saa ya
tisa ambapo mwanafunzi mwenye umri wa miaka 15 alipokuwa anachanja kuni na
wenzake watano.
Inadaiwa kuwa wakati wakiendelea kuchanja kuni alipita mtu
mmoja akiwa amevaa sare za wafungwa na baada ya muda mfupi mtu huyo alirudi
akiwa uchi wa mnyama na akiwa amejipaka masizi kifuani huku akikimbia kuelekea
walikokuwa wakichanja kuni.
Kufuatia hali hiyo walianza kukimbia kila mtu uelekeo
wake huku wakipiga kelele za kuomba msaada lakini kwa bahati mbaya mwanafunzi
huyo alijikwaa na kuanguka chini na ndipo mtuhumiwa alipomvamia na kumbaka.
Imeelezwa kuwa wakati mtuhumiwa akifanya kitendo hicho
mwanafunzi aliyebakwa aliweza kumtambua kwa sura mbakaji.
Baada ya kufanya kitendo hicho mbakaji aliondoka
huku mwanafunzi huyo naye aliondoka kuelekea bahati nzuri alikutana na mtu
mmoja na kumsimulia majanga yaliyomkuta ndipo mtu huyo akampa msaada kwa kumpeleka
kuripoti kituo cha polisi.
Akizungumzia tukio hilo mwanafunzi huyo(Jina tunalo) amesema
kuwa siku hiyo aliondoka na rafiki zake ambao hakuwataja majina yao
kwenda porini kwa ajili ya kuchanja kuni na kumuona mfungwa huyo akaanza
kuwakimbiza.
“Bahati mbaya niliteleza na kuanguka,baada ya kuanguka
ndio akanikmata ana kunivulisha nguo na kunitendea unyama huo ambao umenisababishia
maumivu makali,naiomba serikali kumchukulia hatua kali aliyenibaka”,alieleza
mwanafunzi huyo.
Kwa upande wa mama mdogo anayeishi na binti huyo (Jina
Tunalo)amesema kitendo alichofanyiwa binti yake ni cha kinyama na yeye
pia kuiomba serikali kumchukulia hatua kali mtuhumiwa huyo kwa unyama huo.
Amongeza kuwa
wamempeleka hospitali ya wilaya ya Geita na kupewa matibabu na kuambiwa warudi
mwezi wa 5 ili apimwe tena kama amepata magonjwa ya zinaa kwani baada ya kupima
hawakuona kama amepata maambukizi.
Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Geita Adam
Sijaona amethibitisha kumpokea mwanafunzi huyo tar 27 na kumpatia matibabu
hatimaye akamruhusu kwenda nyumbani
Kamanda wa polisi mkoani Geita kamishina msaidizi
mwandamizi Leonard Paul amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo la mfungwa kubaka
mwanafunzi na amesema kuwa mtuhumiwa ameshakamatwa na jeshi la polisi na
taratibu za kumfikisha mahakamani zinaandaliwa ili akajibu tuhuma inayomkabili.
Inasemekana mfungwa huyo aliyebaka
anatumikia kifungo cha miezi sita jela katika gereza hilo la Butundwe.
Na Valence Robert-Geita