Tukio
hilo lilitokea wiki iliyopita Vingunguti nyumbani kwa Zaina
Athumani,70, ambaye ndiye mwenye nyumba aliyeleta mganga huyo ili
azindike nyumba yake, mwingine aliyepatwa na tatizo hilo ni mpangaji
wake aliyejulikana kwa jina la Haruna Ally.
Vyanzo vyetu vya habari vinadai kwamba Bi mkubwa Zaina alifikia hatua ya kumuita mganga huyo kutokana na kile alichodai kuwa nyumba yake haina kinga ya aina yoyote hivyo wachawi kufanya vituko vyao usiku na sauti za ajabu kusikika hivyo kushindwa kupata usingizi.
Vyanzo vyetu vya habari vinadai kwamba Bi mkubwa Zaina alifikia hatua ya kumuita mganga huyo kutokana na kile alichodai kuwa nyumba yake haina kinga ya aina yoyote hivyo wachawi kufanya vituko vyao usiku na sauti za ajabu kusikika hivyo kushindwa kupata usingizi.
Imeelezwa
kuwa baada ya wapangaji kuingiwa na wasiwasi na sauti hizo walimuomba
mama mwenye nyumba atafute mganga naye aliamua kumleta ili kuwafukuza
watu waliokuwa wakipiga kelele usiku bila kuonekana.
Taarifa
zaidi zilidai kwamba baada ya mganga huyo kufika nyumbani hapo alitoa
vitu mbalimbali vya ajabu katika nyumba hiyo kisha kuwanywesha dawa
watu zaidi ya 20 lakini mwenye nyumba na mpangaji wake mmoja walizidiwa
wakadondoka chini na kuzimia ndipo mganga akaingia mitini.
Imeelezwa
kuwa baada ya wapangaji kumuona mwenye nyumba ulimi umetoka nje
waliangua kilio wakijua kuwa atakata roho, hata hivyo walipiga simu
polisi na kuwaeleza mkasa huo.
Polisi
walifika mara moja na kuwachukua wagonjwa hao na kuwakimbiza Hospitali
ya Amana kwa matibabu lakini mganga akawa amekwishatoweka.
Mwandishi
wa habari hizi alifika nyumbani kwa Bi mkubwa Zaina juzi na kumkuta
akiwa ameshatoka Amana huku Haruna akiwa bado anaendelea na matibabu.
Alipoulizwa juu ya sakata hilo alisema: “Nilikuwa na nia nzuri tu
lakini nashindwa kujua kwa nini mimi ndiyo mambo yamenigeukia.
Bado
najisikia vibaya kwani mwili unauma,” alisema bi mkubwa huyo, hata
hivyo alidai hajui anakoishi mganga huyo kwa sababu alimpata
barabarani.
Credit-Farajimfinanga.info