Inatishaaa!!! NDUGU WA KIUME WAMCHINJA HAWARA WA MAMA YAO KISA WIVU WA KIMAPENZI HUKO KATAVINdugu wawili wa kiume wa familia moja  ambao  ni wakazi  wa Kitongoji cha Milumba , Kata ya Kibaoni ,wilayani Mlele katika mkoa  wa Katavi  wanadaiwa  kumuua  kikatili, Kitungulu Luhende (65)  kwa kumchinja  na kuutelekeza mwili  wake  porini.

Taarifa  kutoka katika  eneo  la tukio  hilo pia kuthibitishwa na polisi  zinadai wa kuwa  chanzo  cha  ndugu hao  wawili  kufanya  unyama huo inadaiwa  ni wivu  waliokuwa  wakimwonea  Luhende ambaye anadaiwa kuwa  hawala  wa mama yao , kwa kufanya na  mama yao  mapenzi  mara kwa mara  tena  bila  kificho .

Inadaiwa  mama yao  aitwae Sai Mponjie (65)  ni mjane  ambapo  kwa muda  mrefu  sasa  amekuwa na mahusiano  ya kimapenzi  na Luhende .

Akithibitisha  Kamanda wa Polisi  wa Mkoa wa Katavi , Dhahiri Kidavashari  aliwataja  wanandugu hao  ni  pamoja na Luhende Kashila (16)  na kakae Nyengu Kashila (19) ambao  wanatuhumiwa kumuua  kikatili  ‘hawala’  ya  mama  yao .

Akisimulia  mkasa  huo , Kidavashari  alidai kuwa  Februari , 22 , mwaka  huu  saa  mbili  asubuhi , Luhende ambae pia  ni mkazi  wa Kitongoji  hicho  cha Milumba  alimwaga  mkewe  ambaye jina lake  halikuweza kufahamiaka mara moja kuwa  anaenda  kijijini Kirida  ambako  pia ana  mji  mwingine .

“Hata hivyo inadaiwa  marehemu  badala  ya kwenda  kijijini Kirida  mwenye  mji  wake mwingine  alipitia nyumbani  kwa rafiki  yake  katika  kitongoji  hicho  cha Milumba , aitwae Milembe Katembeni  ambako  aliiacha pikipiki  yake  yenye aitwae Sai “  alidai Kamanda  Kidavashari.

Inadaiwa kuwa  marehemu  hakuweza kuonekana  tena  hadharani  hadi  mwili  wake  uligundulika  ukiwa umetekelezwa  katika  eneo  la  milima  ya kitongoji  hicho cha  Milumba   ukiwa tayari  umeshaharibika  kufuatia  msako  mkali uliofanywa  na  askari Polisi  na  askari  wa jadi ‘sungusungu’huku pembeni  ya mwili  huo wa marehemu  iliokotwa  leseni  yake ya udereva  Daraja A.

“Baada ya  marehemu kutorejea  kuchukua pikipiki  yake  rafiki  yake  aliingia  wasiwasi  baada ya wiki  kupita  bila Luhende  kuonekana  na kuchukua mali  yake  hivyo aliamua kutoa  taarifa kwa Mtemi  wa  Sungusungu  katika Kitongoji  hicho  kisha  akatoa  taarifa  katika Kituo  kidogo cha Polisi  cha Kibaoni  ndipo msako  mkali ulipoaanza “anadai Kamanda .

Kwa mujibu wa Kidavashari  chanzo  cha mauaji hao  ni  wivu wa watoto  hao  baada ya kuona   marehemu  akifanya  mapenzi  na mama  yao  mara kwa  mara  kitendo  kinachodaiwa  kuwakera  sana  watoto  hao .

Anaongeza  kuwa  tayari  mama ya watoto  hao Sai Mponje (65)  na  mwanae  aitwae Luhende Kashele  (16)  wanashilikiwa  kwa mahojiano  huku  polisi  ikimsaka  mtoto  mwingine  aitwae Nyengu  Kashele (19)  ambaye  alitoroka mara  baada ya  kufanyika  kwa  mauaji  hayo  na kujificha kusikojulikana .
 Na Walter Mguluchuma, Mpanda - Katavi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post