MWANAMKE AJIFUNGUA NDANI YA BASI LA ABIRIA Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanamke mmoja jina halijafahamika anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 20-25 akiwa na mumewe, wakitokea wilayani Chunya mkoani Mbeya
wakielekea wilayani Mbozi amejifungulia kwenye gari aina ya Coaster jana lenye namba T 653 CTC.
Gari hiyo ilikuwa ikielekea Tunduma ambapo imeelezwa kuwa Mwanamke huyo alijifungua mtoto wa kiume.
 
Mwandishi wa habari hizi Moses Ngwa't anasema licha ya yeye kuwa shuhuda wa uzazi huo kwasababu alikaa na mjamzito huyo, Bibi mmoja ndye alikuwa shujaa wa kumzalisha binti huyo. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post