SHUHUDIA HAPA TUKIO LA SHEREHE ZA KUADHIMISHA SIKU YA SHERIA NCHINI ILIVYOFANYIKA KATIKA MKOA WA SHINYANGA LEO

Ni katika viwanja vya Mahakama ya mkoa wa Shinyanga mjini Shinyanga ambako mapema leo kumefanyika sherehe za kuadhimisha siku ya sheria nchini ikiwa na kauli mbiu “utendaji wa haki kwa wakati,umuhimu wa washiriki wa wadau” .Watu mbalimbali  wamehudhuria sherehe hizo akiwemo mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga,wajumbe wa kamati za ulinzi na usalama mkoa,wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa,waheshimiwa mahakimu,mtendaji wa mahakama,mawakili wa serikali na wa kujitegemea,viongozi wa dini,viongozi wa siasa,wakuu wa taasisi za serikali,mashirika ya umma na binafsi,waandishi wa habari,watumishi wa mahakama n.k


Awali Wakili wa kujitegemea John Ng’wigulila akisoma risala kwa niaba ya mawakili wa kujitegemea mkoani Shinyanga ambapo amesema vikwazo wanavyovipata kwa wateja wao ni mahakimu wa mahakama za mwanzo kuzuia mafaili ya mashtaka kwenda mahakama za wilaya kwa ajili ya mawakili kumtetea mteja wao,hivyo kuiomba kuiomba serikali kupitia sheria hiyo ili sheria iwaruhusu wao kwenda moja kwa moja kwenye mahakama za mwanzo  kuwatetea wateja wao ili kusaidia katika suala la kutenda haki kwa wakati kwa wananchi

Wakili  kutoka ofisi ya serikali Mwanasheria mkoa wa Shinyanga  Seth Mkemwa akizungumza katika sherehe za siku ya sheria nchini ambapo pamoja na mambo mengine alisema miongoni mwa vikwazo vinavyochelewesha mashauri/kesi ni dharura kwa wadau

Sherehe zinaendelea
Hakimu mkazi mfawidhi mwandamizi wa mkoa wa Shinyanga John Chaba akizungumza katika sherehe hizo ambapo amesema  siku ya sheria nchini ilianzishwa mwaka 1996, na huashiria mwanzo rasmi wa kalenda ya kuanza kwa shughuli za mahakama nchini kote na hufanyika kila mwaka ikitumika kuwaombea dua pamoja na sala watumishi wa wote wa mahakama hususani watendaji wakuu wakiwemo majaji na mahakimu ili waweze kufanya kazi zao katika misingi ya haki zaidi wakimtumainia mungumiongoni mwa changamoto zinazoikabili mahakama ya mkoa wa Shinyanga ni uhaba na uchakavu wa majengo ya mahakama yanayotumika kwa shughuli za kimahakama.

Mwanasheria mkuu ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi Lightness Tarimo,ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo Ally Nassoro Rufunga katika sherehe za siku ya sheria nchini zilizofanyika katika viwanja vya  mahakama ya mkoa mjini Shinyanga.Akizungumza katika sherehe hizo amesema Idara ya mahakama katika mkoa wa Shinyanga inakabiliwa na changamoto ya uhaba na uchakavu wa majengo ya mahakama uhaba wa mahakimu katika mahakama ya mkoa,wilaya na mwanzo ambapo idadi ya mahakama za mwanzo ni 11 katika wilaya ya Kahama,13 wilaya ya Shinyanga na Kishapu 12 huku ikidaiwa kuwa kwa muda mrefu sasa katika wilaya ya Kishapu hakujajengwa wala kufunguliwa kwa mahakama ya wilaya

Mwanasheria huyo kutoka ofisi ya mkoa wa Shinyanga amesema mkoa wa Shinyanga unatekeleza mpango wa matokeo makubwa sasa,ambapo utekelezaji wa mpango huo unazingatia muda hivyo kutaka mpango huo utumike pia katika kukamilisha jengo la mahakama kuu Shinyanga ambalo ujenzi wake ulianza mwaka 2008/2009 lakini hadi sasa haujakamilika

Wadau wa mahakama wakisikiliza hotuba ya mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga,ambaye alikuwa Mwanasheria mkuu ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi Lightness Tarimo

Burudani ya wimbo kutoka kwa mwandaaji wa wimbo maalum ikiendelea katika eneo la tukio

Wimbo ulikuwa mzuri kweli kweli na miongoni mwa maneno yaliyokuwa ndani ya wimbo ni "Nchi itafanikiwa kama haki itatekelezwa"

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post